WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere

Thursday, March 14, 2013

Neno La Leo; Mwenye Akili Ya Darasani Yumkini Punguani Wa Mtaani!

Photo: Neno La Leo; Mwenye Akili Ya Darasani Yumkini  Punguani Wa Mtaani!
Ndugu zangu,
Nimepata kuandika, kuwa Delirium ni hali ya mwanadamu kuwa katika mkanganyiko ( kuchanganyikiwa). Ni maradhi.
Tunayoyashuhudia sasa ni dalili za kuwa tumo kwenye hali ya Mkanganyiko- Delirium.
 
Katika dunia hii fasihi imetusaidia sana kutujengea uwezo wa kuyapembua mambo. Kuchagua kati ya chuya na mchele.
Wengine elimu yao ni ya darasani tu, mitaani humu tunamoishi haiwasaidii.  Ni kama punguani tu.
Leo katika Tanzania hii kuna watu wanakwenda kuombewa ili wenye kuwadai wayasahau madeni yao. Ni kuchanganyikiwa.
Na tatizo ni hili. Mwanadamu huyu akisimama mtaani na kutamka kwa sauti kuwa anamwomba Mungu wa mbinguni amsaidie anayemdai asahau deni lake, basi, sisi tunaopita njia tutamtazama na kuambiana; " Mwendawazimu yule!".
Lakini, ' mwendawazimu' yule akikusanyika na wengine  wakafika hamsini, na mbele akasimama  anayefanya maombezi, ambaye kimsingi anafanya kazi kama ya ' waganga' wa kienyeji, akitamka; " Nawaombea kwa Mungu enyi mnaodaiwa na NBC au CRDB, Mungu   awasaidie wenye kuwadai wasayasahau madeni yao!"
Hapo tunaopita njia tutaambiana; " Aisee, pale kuna muhubiri anayewaombea wenye kudaiwa wadai wao wayasahau madeni yao!"
Kumbe, lile ni kusanyiko tu la wenye kuota ndoto za mchana. Wenye kuota kuwa NBC au CRDB itayasahau madeni yao waliyokopa.  Na watatokea wengine wenye kutoa ushuhuda wa kusamehewa madeni yao na NBC na CRDB.
Kwenye kitabu cha ' Things Fall Apart' hata Unoka, baba yake Okonkwo anayesemwa kuwa alikuwa dhaifu na mtu ambaye Okwonkwo hakupenda afanane naye, alikuwa na cha kutufundisha. 
Kuwa kwa mwanadamu anayedaiwa lazima atambue kuwa anadaiwa. Kama umekopa ni sharti ulikubali deni lako. Ndio uungwana.
Anayekudai hawezi kirahisi kusahau deni lake. Wakati wewe utaomba kwa Mungu asahau deni lake, naye pia ataomba kwa Mungu huyo huyo deni lake ulilipe!
Wenye kudai kuwa wanaweza kuwaombea wanadamu wengine ili wenye kuwadai wayasahau madeni yao, hao kimsingi wanajipatia fedha kirahisi kutoka kwa wenye kudaiwa. 
Na wengine wenye kudaiwa elimu zao ni za darasani tu, mitaani ni punguani!
Ni Neno La Leo.
Maggid,
Iringa.
<a href=

http://mjengwablog.co.tz/

No comments:

Post a Comment