WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Sunday, March 3, 2013

CCM yamlaumu Maalim kwa kauli ya “ikibidi litote tugawane mbao”

Na Zanzibari Islamic News blog --

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemtupia lawama nzito Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad  kwa kuanza kwenda kinyume na makubaliano yaliounda Serikali ya Umoaja  wa Kitaifa mwaka 2009.

Akihutubia mamia ya wanachama na mashabiki wa CCM waliohuidhuria mkutano wa hadhara uloiofanyika Jumba la Vigae  huko Jang’ombe mjini Unguja leo (3.3.13), Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar, Vuai Ali Vuai amesema Maalim Seif ameanza kufanya vikao vya siri vinavyotishia kuvuruga amani na umoja wa kitaifa Visiwani humu.

Vuia ambaye ni kati ya wajumbe waasisi walioshiriki katika mchakato wa mazungumzo ya upatanishi wa kisiasa Zanazibar, amesema kama angeliijua mapema dhamira ya Maalim Seif katika mazungumzo ya kundwa kwa Serikali iliyopo, angekuwa radhi kujitoa na kutokuwa miongoni mwa wajumbe wa kamati ya muafaka.

Amesema kwamba hivi karibuni kiongozi huyo ambaye ni Katibu Mkuu wa CUF, ameitisha kikao maalum cha vijana wa chama chake na kusema, ikiwa chama chake kitawaamrisha vijana, nchi haitatawalika na ikibidi litote tugawane mbao.

Aidha Naibu huyo Katibu Mkuu amesema msingi wa  mazungumzo ya vyama vya CCM na CUF  katika awamu zote za kusaka maridhiano ya kisiasa yalihimiza kujengeka kwa hali ya amani, utulivu na mshikamano wa kitaifa.

Vuai ameiita kauli hiyo ni ya kichochezi na kwamba haikubaliki mbele ya jamii na kuwatolea wito viongozi wa kisiasa na kiserikali kuchunga ndimi zao ili kuyaenzi mazingira yalioleta maridhiano ya kisiasa.

Amesema Maalim Seif kama anataka litote ili wagawane mbao ni heri akachukua mapema ubao wake na kuelekea Mtwambwe na kwamba CCM haiko tayari kuona kuona amani ya Zanzibar ikichezewa kwa maslahi binafsi.

Naibu huyo  Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar amesema miongoni mwa mambo waliokubaliana katika mchakato wa mazungumzo ya kusaka upatanisha , yamewaaasa wanasiasa kutotoa kauli na matamshi makali yanayoweza kuiparaganya tena Zanzibar.

Amesema kwa muda wa mwaka mmoja CCM kimekuwa hakifanyi mikutano ya hadhara kwa kuheshimu makubaliano hayo lakini  CUF viongozi wake wamekuwa wakiendesha mikutano yenye kejeli na vitisho yanayoweza  kuirudisha nyuma Zanaibar mahali ilikotoka.

Akizungumzia madai ya kuwepo kwa utata wa  Muungano, Vuai amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni halali na kuwataka wanasiasa wanaopotosha jambo hilo kutafakari  kwa kina faida zitokanazo na kuwepo kwake pia athari ikiwa Muungano huo utavunjika

No comments:

Post a Comment