WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Wednesday, March 20, 2013

Neno La Usiku Huu; Ni Lazima Tupande Mbegu!

00 b30a2

Ndugu zangu,

Kwenye moja ya mashairi ya Marcelino Dos Santos wa Msumbiji ( Pichani kulia) anasema; " We Must Plant". Kwa maana ya tuna lazima ya kupanda.

Dos Santos hazungumzii kupanda mbegu za mahindi au mtama, bali kupanda fikra za kimapinduzi kwa wanajamii.

Ni Fikra zitakazowasaidia kutoka katika hali iliyopo na kwenda kwenye hali nyingine iliyo bora zaidi.

Na mwanadamu unafanyaje unapoamka na kukuta dunia unayoishi ardhi yake imeanza kumegeka na kuchotwa na bahari? Kuna niliyemwuliza swali hilo. Naye akanijibu;

” Huo ndio utakuwa mwisho wa dunia!” Aliyenijibu alikuwa amechoka kufikiri. Nilidhani amgetamka, kuwa angeanza kujifunza kuogelea. Maana, kwa kuogelea majini angeweza kukutana na kisiwa, au nchi kavu.

Wanadamu tumejaliwa akili ili tuweze kufikiri. Na kufikiri ndiko njia mojawapo ya kuiteka kweli. Kufikiri kunahamisha milima na hata kuiweka kando kuruhusu mwanga upite.

Inakuwaje basi mwanadamu anapoacha kufikiri? Haya ya ya kuendekeza abrakadabra za Freemasons ni kielelezo cha Watanzania, kama ilivyokuwa kwa Babu wa Loliondo, kuamua kuacha kufikiri. Ndiyo, kuna waliojifunika vilemba vya ujinga. Wako gizani. Wanahitaji mwanga.
 
Ni Neno La Usiku. ( Pichani nilipokutana na Mjamaa mwenzangu, Marcelino Dos Santos, Nairobi , 2007)
Maggid Mjengwa,
Iringa

No comments:

Post a Comment