WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, March 21, 2013

Sherehe Za Kumsimikwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani,

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisindikizwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la  Chakula la Umoja wa Mataifa, FAO Bw. Jose Graziano da Silva baada ya mazungumzo yao wakati alipotembelea  makao makuu ya FAO mjini Roma, Machi 20, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mtaifa la Chakula (FAO), Jose Graziano da Silva wakati alipotembelea Makao Makuu ya Shirika hilo Mjini Roma, Machi 20, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisikiliza jambo kutoka kwa  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la  Chakula la Umoja wa Mataifa, FAO Bw. Jose Graziano da Silva kabla ya kusaini kitabu cha wageni baadae walifanya  mazungumzo yao katika   makao makuu ya FAO mjini Roma, Machi 20, 2013.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  na Mkewe Tunu wakifanya mahojiano na mtangazaji wa Radio Vatican, Padri Richard Mjigwa (katikati)  kweye  moja kati ya studio  za Raido hiyo Mjini Roma walikohudhuria sherehe za  kusimikwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki Diuniani, Papa Francis 1 Machi 20, 2013
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  na Mkewe Tunu wakiongozwa na Padri  Alquine Nyirenda wa Makao Makuu  ya Shirika la Watawa wa Benedikti, Roma kutoka kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro la Roma walikohudhuria  sherehe za  kumsimikwa kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis 1 kwenye viwanja vya Kanisa hiloMachi 19,2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (wapili kulia) wakipata maelezo  kuhusu historia ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro la Roma kutoka kwa Padri Alquine Nyirenda wa Makao Makuu ya Shirika la Watawa wa wa Benedikti, Roma walikohudhuria sherehe za kusimikwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, Machi 202013.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
 
source: Haki Ngowi

No comments:

Post a Comment