WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Friday, March 22, 2013

Serikali, dini, vyama vya siasa kujadili amani

 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amesema serikali itaitisha kikao cha wadau kutoka taasisi za dini, mashirika yasiyo ya kiserikali na vyama vya siasa ili kujadili mustakabali wa taifa na hasa suala la amani na utulivu.

Pinda alisema hayo juzi wakati wa mahojiano maalum na kituo cha Redio Vatican, kilichopo Vatican City, mjini Roma, Italia.

“Serikali inatarajia kuitisha kikao cha wadau wote kutoka vyama vya siasa, mashirika ya dini, NGOs, ili kutafakari nini kifanyike, ambacho kitasaidia kuendeleza amani na utulivu... tutaitisha kikao hiki tarehe 4 Aprili,” alisema Pinda wakati akihojiwa na Padri Richard Mjigwa, Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Redio Vatican.

Akijibu swali kuhusu kuwapo kwa vurugu na mauaji ya viongozi wa kidini nchini, Pinda alisema serikali imechukua hatua za kisheria kwa kufanya uchunguzi wa kina kwa kila eneo na baadhi ya wahusika kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
Alisema juhudi kubwa bado zinaendelea kuwasaka wahusika wa mauaji ya Padri Evarist Mushi, aliyeuawa visiwani Zanzibar.

Mbali na Padri Mushi, viongozi wengine wa dini waliouawa ni Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste Assemblies of God, Mathayo Kachila na Imamu wa Msikiti wa Mwakaje, eneo la Kitope, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Sheikh Ali Khamis Ali.

Wapo pia waliojeruhiwa, akiwamo Padri Ambros Mkenda wa Kanisa Katoliki la Mpendae mjini Zanzibar, aliyejeruhiwa kwa risasi na Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Suleimani Soraga, aliyemwagiwa tindikali na watu wasiojulikana.

Pinda alitumia fursa hiyo kuwaeleza Watanzania walioko ughaibuni, ambao wanaisikiliza Redio Vatican kwa njia ya mtandao hatua, ambayo mchakato wa uundaji katiba mpya imekwishafikiwa kwa sasa.

Alitumia nafasi hiyo kuwaomba Watanzania na watu wenye mapenzi mema kushikamana na waendelee kumwombea Papa Francis I ili afanikishe kazi, ambayo amepewa na Mwenyezi Mungu aikamilishe.

 “Ujumbe alioutoa kwenye misa ya jana (Jumanne) umenigusa sana na hasa msisitizo wake wa kutaka kila mmoja wetu aone atawasaidiaje watu maskini… watu wanaotengwa, watu wanaonyanyaswa na watu wanaonyanyapaliwa.”
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment