WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Friday, March 29, 2013

UJUMBE WA PASAKA 2013: TOSHEKENI NA MISHAHARA YENU:




"Sauti ya mtu imesikika jangwani: `Mtayarishieni Bwana njia yake; nyosheni mapito yake.  Kila bonde litafukiwa, kila mlima na kilima vitasawazishwa; palipopindika patanyooshwa, njia mbaya zitatengenezwa.  Na, watu wote watauona wokovu utokao kwa Mungu."`

"Enyi kizazi cha nyoka! Ni nani aliyewadokezea kwamba mngeweza kuiepuka ghadhabu inayokuja?  Basi, onyesheni kwa matendo kwamba mmetubu”.

Umati wa watu ukamwuliza, “Tufanye nini basi? Akawajibu, Aliye na nguo mbili amgawie yule asiye na nguo; aliye na chakula afanye vivyo hivyo. Nao watoza ushuru wakaja pia ili wabatizwe, wakamwuliza, Mwalimu, tufanye nini?  Naye akawaambia, Msitoze ushuru zaidi ya kima kilichowekwa.  Nao askari wakamwuliza, "Na sisi tufanye nini?  Naye akawajibu, Msichukue vitu vya mtu yeyote kwa nguvu wala kumshtaki yeyote kwa uongo. Toshekeni na mishahara yenu."

Leo natamani kulizungumzia neon hili  Toshekeni na mishahara yenu:

Neno  hili ni zito japo lilizungumzwa kipindi kirefu nyuma lakini tunaendelea kulishuhudia leo tunapowaangalia watendaji wetu katika serikali zetu; Neno hili linatufundisha uadilifu, uwajibikaji kulingana na maadali  na kanuni za kazi ambazo zinatulazimu sisi kama watendaji wa Taifa kuweka mbele matakwa ya Taifa na sio masihahi binafsi;

Najiuliza tena  Neon hili linamaana gani kwa taifa letu? 

Kama nchi na wananchi wake tunahitajii uhuru wa kiuchumi ambao unatokana na viongozi wetu waridhike na mishahara yao; kinyume chake kama hawataridhika na mishahara yoa na kuweka mbele masilahi yao vitendo vya  rushwa na ufisadi ambao unarudisha maendeleo ya Taifa nyuma sana vitadhidi kuendelea.

 
Ujumbe wa  Pasaka ya mwaka 2013  utukumbushe sisi  Kama Taifa na kama Raia na watendaji ambao tumekula kiapo cha utii na maadili bora ya uwajibikaji kwa Taifa letu kuwapa wananchi wanyonge zawadi kubwa ya  uhuru  wa kiuchumi ili kila mmoja wetu aweze kuyafurahia  hii zawadi pekee ya rasilimali  ambayo Mungu amelijalia Taifa hakuna atayepingana nami kuwa  nchi yetu imefurika kwa uwingi wa asali na maziwa tatizo ni huluka ya kushindwa kutosheka na tukipatacho kwa watendaji wetu na kusababisha, wachache tu ambao wanafaidi rasilimali hii tuliyojaliwa na Muumba wetu. 

kwa kipindi kirefu tumeona kuwa nchi yetu  Tanzania iliyokuwa ikifurika neema  ya rasilimali sasa imegeuka; kwa wengine imekuwa ni nchi inayofurika machungu; matendo yaleyale ya kifisadi, ya ukandamizaji, ya unyanyasaji ambao  Farao aliwatendea wana wa Israeli huko misri miaka hiyo; lakini kwa kuangalia falsafa hiyo ya matendo ya Farao ndio tunaona Namna watendaji wetu walikokabidhiwa dhamana ndani ya Taifa letu  ambao sio waadilifu wananyatenda sasa yanaenda kinyume na uhuru tuliopewa kama zawadi kuto kwa Mungu ambao kila mmoja anastahili kufurahia na kufaidi asali na maziwa yanayofurika katika nchi hii. Na sio kwa kikundi kidogo cha watu.

Yohane Mbatizaji kwa usitadhi kabisa anayafafanua makundi yaliyokusanyika kwa kuwaeleza uwiano sahihi wa toba. Kulingana na Yohane matajiri wanaotakiwa kuangalia haki ya masikini, "Aliye na nguo mbili amgawie yule asiye na nguo; aliye na chakula afanye vivyo hivyo."(Lk 3,11), kwa watoza ushuru waepuke rushwa na matendo ya kifisadi "Msitoze ushuru zaidi ya kima kilichowekwa."(Lk 3,13) na kwa maaskari wazingatie haki "Msichukue vitu vya mtu yeyote kwa nguvu wala kumshtaki yeyote kwa uongo.
Toshekeni na mishahara yenu."(Lk 3,14).

Leo hii ndani ya Taifa vitendo hivi vimeshamiri tena kwa kiasi kikubwa katika jamii yetu, na pengine kila mmoja ameshiriki kwa namna moja au nyingine katika uovu huu, moja kwa moja au kwa kutokuwajibika ipasavyo katika eneo lake la kazi na hivyo kusababisha mianya katika kukua kwa matendo haya maovu. Wito wakati tusherekea Pasaka 2013 sisi kama Taifa inatupasa tubadilike na kuhakikisha haki na upendo vinashamiri katika jamii yetu.

Kama tutafanikiwa kuishi kwa ujumbe huu wa Yohani Mbatizaji kuwa tutosheke na mishahara yetu mimi naamini kuwa tukiweka mbele maslahi ya nchi, taifa letu na wananchi wake hasa wanyonge  tutasonga mbele. TUKUMBUKE KAULI YA YOHANA MBATIZAJI KWA WALE ASKARI kuhusu dhuruma:
TOSHEKENI NA MISHAHARA YENU, watu wana madaraka makubwa mishahara mikubwa na masurufu manono lakini bado wanaiibia nchi.

Hebu tujaribu kuangalia kauli ya Mheshimiwa Lusinde alidai kwamba Malipo yetu ni kidogo sana, hayatoshelezi kabisa lakini wananchi tunaowawakilisha hawatuelewi katika hili, maana wanadhani tuna fedha nyingi, sasa hapa kuna tatizo. Nadhani kuwapo utaratibu wa kuwaelimisha, wajue hata kazi nyingine tunazofanya siyo wajibu wetu ila tunajitolea na nyingine hizi zina gharama kubwa.”

Kama mwandishi mmoja alivyowahi andika kuwa “Tatizo la waheshimiwa hawa wakishapata kura wanageuka viumbe tofauti kabisa na wale waliokuwa wakijifanya wana uchungu kweli na wapiga kura wao. Wanasahau kuwa wengi wa wananchi waliowapigia kura waheshimiwa hao kuingia bungeni ni masikini wa kutupwa na hawana wa kumlalamikia (na hata wakilalamika ni kazi bure maana wawakilishi wao nao wapo ‘bize’ kulalamikia mishahara na posho)”.

Je watendaji wetu wako tayari kutoa hesabu za utendaji wao siku watakapotakiwa na Mwenyei Mungu tukiamini kuwa kazi zote hutoka kwa Mungu “Sisi tunajielewa kuwa ni watendakazi wa saa ya kumi-na-moja katika shamba la Bwana la siku za mwisho, na kwamba ingawa mishahara yetu haijulikani na mapema, lakini hatuna mashaka kwa sababu Bwana wetu ni mkarimu”.

Nafiki Pasaka hii kujifunze kitu kingine kipya kuwa “Jihadharini na tabia ya kupenda fedha, na “toshekeni na mlivyonavyo” kwa sababu Mungu mwenyewe alisema,

 “Kwa vyo vyote sitakupungukia kabisa, wala sitakutelekeza na kukuacha bila msaada. Kamwe, kamwe, sitakuacha hata kwa kiwango kidogo, kukuacha bila msaada, au kukuacha, au kukuangusha, au kulegeza mkono wangu kwako. Hakika sitafanya hivyo! Kwahiyo tunafarijika na kutiwa moyo, na kwa uhakika na ujasiri twathubutu kusema, ‘Bwana ndiye anisaidiaye” (Ebr 13:5, 6)

Kwa kutosheka na mishahara yetu na kwa kuamini kuwa sisi ni wachache ambao tumechaguliwa na Mwenyezi Mungu kuwa saidia wengine ili waweze kupata ridhiki zao; au kufurahia asali na maziwa kwa vipaji vyetu kwa kutimiza ibu wetu tutakuwa tunatekeleza ujumbe huu wa “Utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake na hivi vitu vingine vyote mtapewa k maelefu.

Tukitenda kila kitu kwa haki kamwe hatutakosa chochote tunachohitaji  ambacho kitakuwa ziada. Mwenyezi Mungu atakupa namna ya pekee kukidhi mahitaji ya ziada.


Imani yangu ni kama ile ya Paulo kama tutatosheka na mishahara yetu,na kuwajali wanyonge katika Kupata Riziki
zao basi “Na Mungu wangu atawajazeni na kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu…”.

Tunaona mambo mengi yanaendelea ndani ya Taifa letu ikiwa na matokeo ya ubinafsi na ufisadi; tumeshuhudia 


  • matokeo mabaya ya vijana wetu ambao wamefanya mitihani ya kidato cha nne mwaka 2012; na matokeo haya yameitwa ni janga la Taifa; 

  • tunaendelea kushuhudia huduma za afya ambazo hazikidhi kiwango kwa wananchi wanyonge

  • tunaendelea kushuhudia mauaji ambayo yanaendelea ndani ya jamii yetuna mengine mengi. 

Kwa nini haya yote yanatokea jibu ni moja tu watendaji wetu hawatosheki na mishahra yao na hawan muda wa kulisaidia Taifa wako bize na shughuli binafsi ambazo ziko nje ya maadili na hata hawana muda wa kuangalia mitaala mizuri ya elimu ya vijana wetu huu ni mfano mdogo tu.

"Mungu hatakosa kuwajazi wale wote wanaoifanya kazi yake sawasawa na mapenzi yake" huu ndio ujumbe wa Pasaka 2013

Emmanuel  Turuka
Kalamazoo Michigan
madobole@gmail.com

No comments:

Post a Comment