WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere

Saturday, March 9, 2013

NENO FUPI LA USIKU HUU; MCHOYO AKIZIDISHA UCHOYO MWISHO HULALA NA NJAA!

Photo: Neno Fupi La Usiku Huu; Mchoyo akizidisha uchoyo mwisho hulala na njaa!
Ndugu zangu,
Uchoyo ni hulka ya mtu. Uchoyo si jambo jema. Na mchoyo akizidisha uchoyo wake mwisho hata yeye mwenyewe hulala na njaa.
Maana,itatokea  nyumbani kwake atafika mgeni aliyeshiba. Mchoyo ataona tabu kupika chakula na mgeni naye ale. Anaweza kuhangaika na vikombe vya chai akisubiri mgeni wake aondoke.
Usiku mwingi utaingia, mgeni ataomba alale kwa mwenyeji wake. Mchoyo ataona aibu kumnyima hifadhi mgeni wake.
Lakini, kwa vile ana hulka ya uchoyo, na anaona tabu kupika chakula na mgeni wake naye ale, basi, mchoyo naye anaweza kulalia kikombe cha chai huku mgeni wake akiwa amelala na shibe!
Ni Neno La Usiku Huu. ( Pichani ni chai yangu ya usiku huu, HAIHUSIANI na Neno hili!)
Maggid,
Msamvu.

No comments:

Post a Comment