WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Wednesday, March 6, 2013

KUFUATIA KUVAMIWA NA KUUMIZWA VIBAYA KWA MWANDISHI ABSALOM KIBANDA

Kibanda akiwa wodi ya wagonjwa mahututi (ICU).
 Baadhi ya majeraha aliyoyapata Kibanda.
Kibanda akiendelea kupata matibabu ICU.
Waziri wa Afya, Dk. Hussein Mwinyi, akimjulia hali Absalom Kibanda katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Magazeti ya Habari Corporation, Hussein Bashe, akimpa pole Kibanda.
Dk. Reginald Mengi (kushoto) akibadilishana mawazo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.
 Dk. Reginald Mengi (kushoto) akibadilishana mawazo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.
 Mwenyekiti wa makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi (kulia) akimpa pole, Afisa Mtendaji Mkuu wa Magazeti ya Habari Corporation, Hussein Bashe.
Wanahabari wakimjulia hali Kibanda pamoja na kupata machache kutoka kwake.Picha na Richard Bukos na Haruni Sanchawa-GPL
---
 MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Habari Corporation, Absalom Kibanda, usiku wa kuamkia leo amevamiwa na watu wasiojulikana wakati akivuka geti kuingia nyumbani kwake na gari yake aina ya Nissan. 

Wavamizi hao walivunja kioo cha gari lake na kumchomoa ambapo walimpiga mapanga na kumjeruhi vibaya jicho la kushoto. Baada ya kufanyiwa unyama huo Kibanda alikimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa matibabu ambapo amelazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi ‘ICU
 
SOURCE: Haki Ngowi blog

No comments:

Post a Comment