WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Saturday, March 9, 2013

Rais Jakaya Kikwete amemtumia salamu za pongezi nyingi Rais Mteule wa Jamhuri ya Kenya, Mheshimiwa Uhuru Kenyatta.




Rais Jakaya Kikwete
--
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jayaka KMrisho Kikwete amemtumia salamu za pongezi nyingi Rais Mteule wa Jamhuri ya Kenya, Mheshimiwa Uhuru Kenyatta.

Katika salamu hizo zilizotumwa leo, Jumamosi, Machi 9, 2013, saa chache baada ya kuthibitishwa rasmi kuwa Mheshimiwa Kenyatta ameshinda Uchaguzi Mkuu wa Kenya uliofanyika mwanzoni mwa wiki hii Jumatatu, Machi 4, 2013, Rais Kikwete amemwambia Mheshimiwa Uhuru Kenyatta:

“Mpendwa Rais Mteule na Kaka, ilikuwa ni furaha kubwa kwangu kupokea taarifa ya ushindi wako wa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya. Niruhusu, kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Tanzania, na kwa hakika, kwa niaba yangu binafsi kukupogenza kwa dhati ya moyo wangu kwa mafanikio haya makubwa ya kuchaguliwa kwako.”

Ameongeza Rais Kikwete: “ Ushindi huu ni ushahidi na ishara ya wazi kabisa ya imani na matumaini ambayo wananchi wa Kenya waliyonayo katika uongozi wako. Huu ni utambuzi wa kazi yako maridadi na mchango wako mkubwa ambao umeutoa katika nafasi mbali mbali za uongozi katika siku za nyuma katika jitihada zako za kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii na ustawi wa nchi yako na wananchi wake.”

Amesisitiza Rais Kikwete: “Wakati unajiandaa kuchukua madaraka ya juu zaidi katika nchi yako, napenda kukuhakikishia msimamo wake binafsi pamoja na ule wa Serikali yangu wa kuunga mkono Serikali yako. Ni imani yangu kubwa kwamba pamoja tutaweza kuendelea kusukuma mbele zaidi maendeleo ya nchi zetu – Kenya na Tanzania na pia utengamano wa Afrika Mashariki kwa manufaa ya nchi zetu na wananchi wake.”



Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

IKULU

DAR ES SALAAM

No comments:

Post a Comment