WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Friday, February 15, 2013

Watanzania wengi hawataki Muungano uvunjwe’



UTAFITI wa Taasisi ya Utafiti kuhusu Kuondoa Umaskini (Repoa), kuhusu mabadiliko ya katiba, muungano na madaraka umeonyesha kuwa asilimia 40 ya Watanzania wanataka Bunge lisimamie mchakato mzima wa mabadiliko ya kupatikana Katiba Mpya.

Pia, utafiti huo umebainisha kuwa asilimia 88 ya Watanzania hawataki muungano uvunjwe huku asilimia 23 wakitaka muungano huo uvunjwe.


Mtafiti Mshauri wa Repoa, Costantine Manda alibainisha hayo jana wakati wa uzinduzi wa utafiti huo uliofanyika kati ya Mei 27 hadi Juni 30 mwaka jana.


“Utafiti wetu umetokana na maswali waliyoulizwa watu wa kada tofauti wapatao 2,400 ambapo mbali na asilimia 40 kutaka Bunge lisimamie kupatikana Katiba, asilimia 25 wanataka Rais ndiye asimamie huku asilimia 18 ikitaka vyama vya kiraia, asilimia 9 ikitaka mahakama na asilimia 6 ikitaka vyama vya siasa vifanye hivyo,”alisema Manda.Alisema mbali na kuangalia upande huo pia wananchi asilimia 54 wametaka mawaziri wote wasitokane na wabunge,hivyo uwekwe utaratibu katika Katiba Mpya ya jinsi ya kuwapata mawaziri hao.


Manda alisema pia waliangalia watu kama wana maoni juu ya Rais kuongoza kwa awamu mbili au la na kati ya wananchi hao waliohojiwa asilimia 87 walieleza kuwa aongoze kwa awamu mbili huku asilimia 12 wakitaka asiwe na ukomo wa kuongoza.


“Wengi wanaonyesha kuwa wanataka Rais aongoze kwa awamu mbili ila kuna wengine ambao wanapinga hilo kama mnavyoona kwenye utafiti wetu,”alisema Manda.


Hata hivyo alisema wananchi asilima 85 wanakubali kufanyika kwa mabadiliko ya katiba iliyopo na kati yao asilimia 71 wanasema ni muhimu iwe hivyo kwa kuwa nchi inakoelekea hivi sasa ni kubaya.


“Lakini kuna wengine asilimia 19 wanaridhishwa na jinsi nchi inavyoongozwa hivi sasa na demokrasia iliyopo,”alisema Manda.

source: Mwananchi

No comments:

Post a Comment