WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Wednesday, February 20, 2013

NINI CHANZO CHA MATOKEO MABAYA YA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012

Picture

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa (Mb) akimuelekeza jambo Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo. Mh Philipo Augustino Mulugo kabla ya kuanza kutangaza matokeo ya kidato cha nne mbele ya baadhi ya wanahabari wa vyombo mbalimbali, kwenye makao makuu ya ofisi za wizara hiyo jijini Dar es Salaam
Mitihani ya Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) kwa mwaka 2012 ilifanyika nchini kote kuanzia tarehe 8-25 Oktoba 2012.  Napenda kuchukua nafasi hii kutangaza rasmi matokeo ya mitihani hiyo kama ifuatavyo :



TATHMINI YA UFAULU WA WATAHINIWA WA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012

8.1           Tathmini ya awali iliyofanyika kuhusu ufaulu wa watahiniwa katika shule mbalimbali inaonesha kuwa shule zilizofanya vizuri zaidi ni zile ambazo zina mahitaji yote ya msingi ikiwemo walimu wa kutosha, miundombinu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia. Aidha, shule zenye ufaulu wa chini ni zile ambazo zina changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na:

(i)         Baadhi ya shule za vijijini hazina kabisa walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati na pia zina upungufu mkubwa wa walimu wa masomo mengine;

(ii)        Kutokuwepo kwa maabara kwa shule zenye mikondo ya sayansi na pia kutokuwepo kwa maktaba kwa ajili ya kujisomea; na

(iii)       Upungufu mkubwa wa vitabu vya kiada na ziada. Katika baadhi ya shule uwiano wa kitabu kwa mwanafunzi ni 1:10.

8.2           Mkakati wa Serikali ni kuendelea kupunguza changamoto hizo kila mwaka ikiwa ni pamoja na kufanya mambo yafuatayo:

(i)             Kuajiri walimu kila mwaka ili kuondoa upungufu uliopo katika shule zetu. Mwaka 2011/2012 Serikali iliajiri walimu wa sekodari 13,246 na mwaka huu wa fedha 2012/2013 imeajiri walimu 12,973 ambao wamepangwa katika shule zenye upungufu mkubwa wa walimu. Ajira ya walimu wapya mwaka huu umetuwezesha kuwa na wastani wa walimu 2-3 kwa shule. Hali hii itaendelea kuboreka kadri tunavyoendela kuajiri walimu.

(ii)            Kuboresha miundombinu iliyoko katika shule zetu ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba za walimu, madarasa na maabara. Mwaka 2012/2013 Serikali imepanga kuboresha miundombinu katika shule 264 zilizopo katika mazingira magumu ikiwemo miundombinu ya maabara na nyumba za walimu.

(iii)           Kuendelea kutoa ruzuku ya Tsh 25,000 kwa mwanafunzi kwa mwaka, ambapo asilimia 50 ya fedha hizo ni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia ili kuziwezesha shule kununua vitabu pamoja na vifaa vingine muhimu kitaaluma.

(iv)           Wizara kuendelea kuzishauri Halmashauri kuweka mgawanyo mzuri wa walimu waliopo baina ya shule na shule.

(v)            Wizara itaendelea kuimarisha Idara ya Ukaguzi wa Shule pamoja na kuwawezesha Waratibu Elimu Kata na Wakuu wa Shule kufanya ukaguzi wa ndani katika Shule za Sekondari zilizo katika maeneo yao.

Source: http://www.wavuti.com/

UCHAMBUZI WA UKADIRIFU:

ELIMU NI HAKI YA MSINGI KWA WANAFUNZI WETU.
Jedwali hapo chini linaonyesha matokeo ya hivi karibuni ya kidato cha nne, matokeo haya yameleta simanzi kwa wananchi wengi ambao wameyaita ni janga la taifa letu kutokana na ukweli kuwa kiwango cha kufeli kimekuwa ni kikubwa mno katika matokeo haya ya kidato cha nne ya  mwaka 2012

Mchanganuo wa ufaulu kwa kila Daraja kwa jinsi kwa Watahiniwa wa Shule mwaka 2012 ni kama ifuatavyo:
DarajaIdadi ya WavulanaIdadi ya WasichanaJumla
I1,0735681,641
II4,4561,9976,453
III10,8134,61315,426
I-III16,3427,17823,520
IV64,34438,983103,327
0120,664120,239240903


Maswali mengi yameulizwa kwa nini taifa limefikia katika hali kama hii; je lawawama ziende kwa serikali kwa kushindwa kutoa kipaumbele katika mfumo mzima wa elimu ya watoto wetu? Au ni tatizo la wanafunzi wetu (watoto wetu) kuto kuwa makini katika masomo yao (lack of seriousness)? Lakini tatizo hasa nini wakati taifa linafahamu wazi kuwaELIMU NI HAKI YA MSINGI?


Ni ukweli ambao haufichiki kuwa Tanzania haitaweza kuendelea na kustawi bila kuwa na elimu nzuri kwa watoto wetu ambao ndio msingi wa kesho wa mustakabli wa taifa letu. Hata kama tutakataa kwa msingi wowote ule ukweli utabaki pale pale kuwa  elimu yetu tukilinganisha na mifumo ya elimu ya nchi nyingine hasa zile ambazo zimeendelea na hata pengine zinazo endelea kama Tanzaania au zinazotuzunguku mfumo wetu wa elimu sio mzuri


Serikali inanadi vipi sera za elimu bora?

Serikali inatueleza kuwa katika miaka 50 ya uhuru imefanikiwa kupanua fursa za watoto na vijana wetu wengi sana kupata elimu ya awali, msingi, sekondari, ufundi na elimu ya juu.
  
Na kwa kutambua mafanikio haya yote  serikali bado inaendelea kutoa kipaumbele cha kwanza kwa bajeti ya elimu ili iweze kuajiri walimu wengi zaidi, kuongeza vitabu na vifaa vya kujifunzia na kufundishia

kuongeza matumizi ya teknohama katika utoaji wa mafunzo pamoja na kujenga uwezo wa wanafunzi na waalimu kiteknolojia ili kwenda sambamba na karne hii ya utandawazi.  
Aidha, inaendelea na mpango wake wa kujenga maabara za sayansi katika sekondari zetu zote. 

Serikali imesisitiza adhima ya kuchuakua hatua thabiti za kuboresha maslahi na mazingira ya kufanyia kazi ya walimu na watumishi wa sekta ya elimu.  

Serikali imekusudia kutenga pesa za kutosha katika kufikia malengo haya.

Tatizo liko wapi?


  • Msongamano wa wanafunzi katika shule zetu ambao hauendani na bajeti inayotolewa, vifaa vya kufundishia; vyumba vya kusomea ambavyo vitaweza kuwagawanya wanafunzi katika idadi ambayo ni rahisi kufundishika na kuelewa na kusaidiwa; Hivyo hushusha kiwango bora cha elimu;    


  • Ubovu wa huduma za jamii kama barabara, hospitali, maji safi na salama; ukosefu wa mishahara mizuri ya kuwamotivate walimu zaidi  kuingia katika taaluma hii; ni kweli kuwa  elimu ni silaha pekee ambayo inaweza kutusaidia kubadilisha dunia na maisha yetu, kwa msingi huu wale ambao wana elimu  sio tu elimu bali elimu bora  wananafasi kubwa ya kufanikiwa;

Je sisi tunataka nini?

Taifa linahitaji utekelezwaji wa haki hii ya msingi kwa vijama wetu yaani:

Elimu bora ambayo inatokana na walimu bora ambao wameshiba na wameridhika ma maisha yao kwa kupata haki zote wanazostahili kupata na wanawajibika kwa moyo bila mashaka

Mitaara ya elimu itayarishwe iendane na masomo yanayolingana na hali halisi ya maendeleo ya dunia ya sasa pamoja na masomo ambayo yanawavutia wanafunzi kujitafutia zaidi jitihada za kusoma?

Sababu nyingine zinazowafanya watoto wetu wasifanye vizuri shuleni ni pamoja na wanafunzi kuchukia shule kutokana na sababu za kitaaluma na kimazingira, shule zetu nyingi zina kosa vifaa muhimu ya kufundishia na kujifunza shule kama inakosa vitabu vya kiaada vifaa vya mahabara je unategeme kuwa kutakuwa na ubora wa elimu hapo? Mimi nasema hapana na tusitegemee miujiza kutoka katika shule zetu za serikali ambazo watoto wetu wengi ndiko wanakosoma.

Pale tutakapo amua kuacha maneno na kuanza kutekeleza maneno yetu kwa vitendo ndipo tutegemee kuona: watoto wetu wakifikia malengo yao ya elimu kupitia elimu bora na kufanikiwa kuondoa umasikini kwa kiwango kikubwa sana.

Pengine kwa akili tu ya kawaida tunaweza kusema kuwa serikali yetu inahusika katika kuharibu mfumo mzima wa elimu, kwa nini nasema hivi kwa msingi huu mmoja mkubwa elimu inapasa iwaguse na kuwahusu moja kwa moja watoto wetu; mahitaji yao yanatakiwa yatiliwe mkazo kwanza kabla ya mambo mengi ya serikali,

Inatakiwa mtoto wa kitanzania kwenda katika shule nzuri inatakiwa iwe ni haki yake ya kikatiba, watoto wafundishwe na walimu ambao ni wazuri ambao wanapokea mishahara mizuri na wanavifaa vizuri vya kufundishia

KWA NINI SHULE BINAFSI ZINAFANYA VIZURI?

Nini kinatokea katika shule za binafsi wana walimu wazuri ambao wanalipwa vizuri na wanavifaa vya kutosha sasa nini tutegemeenini kutoka katika shule kama hizi ni wazi kuwa matokeo yao ya mitihani itakuwa ni daraja la kwanza na watoto wakifeli ni daraja la pili;    

katika mafanikio ya ufaulu wao wazazi nao wanamchanga mzuri sana  katika maendeleo ya watoto wao, wazazi wanahusishwa katika maswala ya kitaaluma na ya kijamii sambamba na watoto wao;  mzazi anajua  ratiba ya kitaaluma na maendeleo ya mtoto/mwanafunzi utaratibu wa shule unampa nafasi ya pekee kama mwalimu jamii ambaye anaendeleza nidhamu na tabia ya usomaji wa mtoto/mwanafunzi nje ya mazingira ya shule na katika maisha ya kawaida ya mtot ndani ya familia;

Kama Taifa tukifanikiwa kufikia hatua kama hii kama shule hizi na jamii nyingine zilizoendela zinavyofanya tutakuwa tumesonga mbele katika mafanikio ya elimu ya watoto wetu; ni kitu kizuri kuona wazazi wakishiriki moja kwa moja katika maisha ya kawaida ya watoto wao na mtoto/mwanafuzni asipomwona mzazi wake katika maswala mbalimbali ya shule anasikitika na  ndani ya demokrasia ya mtoto mwenye nidhamu anamuuliza mzazi wake Baba/Mama leo hujeangalia kazi zangu au leo hukuja katika michezo yetu na hukufanikiwa kuniona jinsi nilivyocheza vizuri, hali hii hatimaye inamwumiza mzazi  na inajenga uwajibikaji wa wazazi kwa watoto wao na kuleta ufanisi mzuri wa kitaaluma shuleni.

Shule zetu zisijikite sana katika maandalizi ya mitihani tu zijikite vile vile katika kuwasaidia watoto wetu katika kujiandaa na maisha yao.

JE WANAFUNZI WANAOSOMA SHULE ZA KATA WANA HAKI SAWA NA WALE WA MIJINI? JE TUNAJADILI PIA MATOKEO YA SHULE ZA KATA/VIJIJINI?

Je shule zetu za vijijini zinafikiwa vipi katika maendeleo ya elimu?
Tunafahamu kuwa wazazi wetu wengi ambao wako vijijini hawawezi kuwasaidia watoto wao kwa vile hata wenyewe wahajeelimika vyakutosha na hata wakati mwingine wanaona aibu kujadili mambo ya shule kwa vile hawajui;

Matokeo yake wanafunzi wengi wanajikuta wakishiriki zaidi katika shughuli za kilimo ( Elimu ya Kujitegemea na kuwafanyia walimu wao kazi majumbani);

  
NINI KINAWAFUKUZA WALIMU WAZURI KAMA WAKO KATIKA SHULE ZA KATA/VIJIJI?

Kutokana ubovu na huduma duni za jamii si rahisi kuwapata walimu bora kwenda kufundisha vijijini wengi watapendelea kubaki mijini;

Hata serikali inajikuta katika wakati mgumu wa kupeleka huduma kama vitabu, nafasi nyingi ambazo zimezcha wazi kutojaza mara moja, hata pale zinapojazwa zinakuwa na walimu ambao sio wazoefu na wazuri kitaaluma.

Ni mara nyingi sana walimu ambao wanfundisha katika shule za vijijini wanaweza wakawa wanafundisha muda mfupi ukilinganisha na wenzao wa mijini kutoka na sababu kama vile wanatakiwa kutembea umbali mkubwa kwa ajili ya kwenda kutibiwa, kuchukua mishahara, kwa ajili pengine ya kwenda kwa ajili ya mafunzo ya  au kutembelea familia zao;

Wlimu wengi wanakuwa hawana nyumba za karibu na shule pengine na wakati mwingine inawapasa kutembea kwa miguu umbali mkubwa kwenda kufundisha asubuhi hali hii inaweza kusababisha kuanza vipindi kwa kuchelewa;
Swala la ukaguzi na utendaji wa walimu ni tatizo pia kutoka na tatizo sugu la usafiri hata wakaguzi hawatembelei shule hizo kuona maendeleo yake mara kwa mara;

HITIMISHO

Lazima tukubali kuwa kuwa na walimu bora ambao wanavifaa vinavyotakiwa kwa ajili ya elimu bora huleta tofauti kubwa sana kwa wanafunzi wetu na sifa kubwa kwa taifa letu; taifa lisipokuwa tayari kubadilika tutaendelea kunyosheana vidole kuhusu matokeo ya wanafunzi wetu kila mwaka kama jedwali la hapo chini linavyoonyesha, kwa ujumla ni aibu kubwa kuona watoto wetu wanafeli kwa kiasi kikubwa namna hii, na kubaliana na wengi ambao wamediriki kusema kuwa hili ni janga la kitaifa ni vyema kama tulitafutia ufumbuzi wa haraka; washauri wa serika li yetu mnashauri nini?

Na lazima tukubali kuwa elimu bora kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu ni haki ya kila mwanafunzi katika jamii hii ya kitanzania; viongozi wetu wanapaswa kulijua hilo na kulielewa hilo na kulitekeleza kwa moyo woto na kwa faida ya wote;

Swali la kujiuliza ni hili pamoja na faidia zote zitokanzao na elimu, kwa nini serikali yetu bado haioni faida ya kuwekeza zaidi katika elimu? “Imesahau kuwa Elimu ni mtaji wa msingi kwa jamii?” Je serikali inaogopa kuwekeza kwenye elimu kwa sababu ya ushindani kutoka kwa wananchi katika kuwaongoza? Ni ukweli kuwa jamii ikiwezesha kwa elimu bora matokeo yake ni kuwa hawatakuwa tayari kukubali kuburuzwa na kudanganywa danganya pengine na sera ambazo hazieleweki;

MUNGU IBARIKI TANZANIA  NA WAPE HEKIMA ZAIDI VIONGOZI WETU KWA KUSHIRIKIANA NA WAZAZI WAWEZE KUTUTOA HAPA TULIPOKWAMA KIELIMU KWA FAIDA YA TAIFA HILI;

No comments:

Post a Comment