WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Wednesday, February 13, 2013

JK: Waliohusika katika mapigano ya kidini kushughulikiwa


NA SHARON SAUWA

Rais Jakaya Kikwete

Siku moja baada ya kuuawa Mchungaji wa Kanisa la TAG mkoani Geita, Mathayo Machila (45),  Rais Jakaya Kikwete amesema mgogoro wa dini ni fedheha na kwamba serikali itawashughulikia wote waliohusika.

Aliyasema hayo mjini Dodoma jana alipokuwa akiwatambulisha wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa wanachama.

Aliwataka Watanzania kuishi kama mwanzo walivyokuwa wakiishi kwa kuvumilia na kila mmoja kuheshimu hisia za mwenzake.

“Hatujawahi kupigana Waislamu na Wakristo kwa masuala ya dini, lakini  jana (juzi) lilitokea na maisha ya watu yalipotea, ni jambo la fedheha na la kusikitisha,” alisema na kuongeza: “Serikali tutaendelea na yale yanayotuhusu kulinda amani, kubaini wachochezi na kuwashughulikia.”

Alisema viongozi wa dini wana mchango mkubwa katika masuala yanayohusu amani na kwamba watakapowaambia waumini wao jambo watafanya na wakiwaeleza wasifanye hawatafanya.
Alitaka kujiuliza ni kwanini tumefika hapa na kuhakikisha kuwa mambo hayo hayatatokea tena.

“Cha msingi tujiulize tumefika hapo na kwanini tumefika hapo?” alihoji na kuendelea: “Kwani vita ya dini haina mshindi kwani kila mmoja yuko sahihi kwa imani yake, hamuwezi kupata mshindi.”

“Tumeishi kwa zaidi ya nusu karne, tukiwa watulivu hivyo tusiruhusu vitendo vya aina hiyo kuharibu utulivu wetu. 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment