WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere

Monday, February 18, 2013

NENO LA LEO: “ I AM SORRY!”

  • i
  • Photo: Neno La Leo: “ I AM SORRY!”
Ndugu zangu,
Neno ‘ Nisamehe’ ni neno fupi sana. Kutamka hilo kwa kimombo ni kusema; “ I ‘m sorry!”
Hata hivyo, neno hilo ni moja ya maneno magumu sana katika lugha nyingi za walimwengu. Neno hilo lina maana kubwa kwa mwanadamu. Laweza kufanya miujiza ya kuwaunganisha watu waliotengana na hata kufikia kuchinjana. Ni pale tu linapotamkwa na mtu mwuungwana na mwenye dhamira ya dhati.
Katika dhambi anazoweza kufanya mwanadamu hapa ulimwenguni, dhambi ya ubaguzi ni moja ya dhambi mbaya kabisa.
Mwalimu Nyerere alipata kutamka; “ Dhambi ya ubaguzi ni sawa na dhambi ya kula nyama ya mtu, ukishaanza kuila tu, basi, hutaacha!” 
Na katika dunia hii ubaguzi hujengwa katika mifumo. Afrika Kusini enzi za Ubaguzi wa rangi walijenga misingi ya ubaguzi. 
Ni kwa kupitia sheria za kibaguzi zilizopitishwa na Bunge.  Kati ya sheria hizo ni pamoja na marufuku ya weusi kukutana, kufanya mikutano na maandamano,  marufuku ya kupata habari na hata kuchapisha habari na mengineyo. 
Lakini, katika dunia hii, himaya zote huporomoka, hata Roma pia iliporomoka. Na himaya ya utawala wa kibaguzi ikafikia hatima yake.
Na kikubwa kabisa kilichowafanya weupe kwa weusi wa Afrika Kusini kuacha ya nyuma na kwenda mbele kwa pamoja ni neno fupi la ‘ I’m  sorry!”- Samahani.
Aliyekuwa kiongozi wa kibaguzi wa Afrika Kusini , De Klerk alisimama mbele ya wanahabari wa dunia na kutamka; “ I am sorry!”. Kwa yote waliyotenda huko nyuma, ikiwamo aliyotenda yeye kama kiongozi. 
Naam, hata hapa kwetu, dhambi ya ubaguzi inaendelea kututafuna. Ni nani mwenye ujasiri wa kusimama mbele ya umma na kutamka; “ I’m sorry!”?
Ndio, huko nyuma TANU na baadae CCM viliamini kuwa
asiyefikiri kama wao basi si mwenzao. Ni mpinzani, ni adui wa maendeleo.
Ni adui wa umma. Ni msaliti. Si mwenzao na alibaguliwa. Alitengwa na pengine kuishia kifungo cha ndani au cha nje. Ni kwa kurudishwa kijijini alikozaliwa au asikozaliwa.
Huko Mtanzania huyo aliyebaguliwa kisiasa. Alifikia kuambiwa kuwa kila siku awe anaripoti kwa Balozi wa Nyumba Kumi. Na kutoka kijijini kwake kwenda kijiji kingine ni sharti aombe ruhusa ya uongozi wa kijiji!
 Na kutoka nje ya wilaya ni sharti apate kibali cha DC! Hii nayo ni historia yetu. Ili tuelewe tulipo na tunakokwenda tuna lazima ya kuipitia
historia yetu.
Ubaguzi wa kisiasa ni jambo baya sana. Migoro mingine inayoibuka kwenye jamii kama hii ya kidini yaweza pia kuwa chanzo chake ni ubaguzi wa kisiasa. Kwamba kuna wanaonyimwa nafasi za kushiriki siasa na kuamua kutumia majukwaa ya kidini kutimiza malengo yao.
Kwamba kuna wanaojiona wao wana haki zaidi kuliko wenzao katika nchi hiyo hiyo ambayo wenzao pia wanaiiita nchi waliyozaliwa. Hivyo, wanawakandamiza wenzao.
 Kwamba wanajiona wana uwezo wa kuwafanya Watanzania wenzao waishi maisha magumu kwa vile tu wanatofautiana au wanapingana kifikra na walio kwenye mamlaka ya dola au Chama kilicho madarakani. 
Ubaguzi wa kisiasa huzaa chuki ya kisiasa. Na mara zote, uvumilivu wa wanaobaguliwa na kukandamizwa hufikia kikomo. Na yanapolipuka, basi, huwa kama nusu ya kiyama. Moto huwaka. Hakukaliki.
Kule Misri vijana wengi wanajua sasa ni kwanini wazazi wao walihangaika sana kutafuta ajira lakini hawakupata. Waliishia  kuishi maisha magumu.
Wanajua sasa ni kwanini baadhi yao ( Vijana) hawakupata scholarship au ajira baada ya kufuzu masomo yao. 
Wanajua sasa, kuwa Idara ya Usalama wa Taifa chini ya Hosni Mubarak, familia yake na jamaa zake wa karibu walikuwa na faili maalumu yenye orodha ya majina ya WaMisri, vijana kwa watu wazima, ambao walionekana kuwa ni wenye fikra za kipinzani. 
Kuna waliochunguzwa tangu wakiwa kwenye mijadala ya vyuo vikuu. Na ambaye jina lake limeingizwa kwenye faili hilo, basi, ataandika kurasa kwa maelfu za barua za maombi ya
kazi, na atasaga lami sana hadi soli za viatu ziishe akitafuta ajira bila mafanikio. 
Serikali ya Hosni Mubarak ilikuwa na mikono mirefu, na miguu pia. Tatizo lilikuwa kwenye ‘kichwa cha Serikali’. Kilikuwa kidogo sana, maana hatma ya yaliyomfika Hosni Mubarak ingepaswa kuepukwa na mtu mwenye kichwa kinachofikiri. Kwa vile kilichotokea kingetokea, ilikuwa ni suala la wakati tu.
Ndio, Usalama wa Taifa ( Zaidi Usalama wa Hosni Mubarak na Chama chake) ulihakikisha Mmisri ambaye jina lake limo kwenye kitabu chao hapati kazi yeyote ile,  labda iwe ya kubeba zege ili hali ana digrii ya chuo Kikuu. 
Ndugu zangu,
Moja ya faida ya kuwa mtu mzima ni ukweli kuwa huhitaji kuliangalia kila jambo kupitia darubini. Mengine utayaona kwa kutumia uzoefu tu.
Ndio, tunajenga nyumba moja, lakini tunagombania fito. Ni hulka za ubinafsi. Na tunaweza kwenda mbele kama taifa, kwa kuyaongea kwa uwazi ya nyuma. Kuyabaini mapungufu yetu, na  kuwa na ujasiri wa kutamka; “ I’m sorry!”
Na hilo ni Neno La Leo.
Maggid Mjengwa,
Iringa,
0788 111 765
<a href=

No comments:

Post a Comment