WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Saturday, February 16, 2013

BUNGE LA KIKOMUNISTI LAZINDULIWA DODOMA


2-wakipinga  3a972
Bunge la Kikomunist Lazinduliwa
Huko Dodoma
Ni habari za kusikitisha na kuhuzunisha kuona kwamba taratibu za ukomunist ambao ulipigwa
marufuku kote duniani mwaka 1991 leo hii bunge letu limezindua mikakati ya kuliendesha
bunge kwa kutumia taratibu za kikomunist! Baadhi ya makala zangu za nyuma nimewahi
kuelezea kwamba moja ya silaha zinazotumiwa sana na wakomunist ni kutengeneza mazingira
ya usiri kati ya watawala na watawaliwa, kwa vile watawal;a siku zote hawapo sahihi na
wala hawajiamini mbele ya watawaliwa ambao ndiyo wananchi waliowaweka madarakani.
Wakomunist wanapangiwa waseme nini!? Waende wapi na wapi wasiende!? Wavae nini na nini
wasivae!? Wale nini na nini wasile!? Wafikiri juu ya nini nakadhalika!

Siamini kwamba katibu wa bunge Dr. Thomas Kashililah alitafakari kabla hajaozungumzia
hoja yake ya kutaka vikao vya bunge visirushwe moja kwa moja, nasema hivyo kwa vile
sababu alizozitoa si sababu za kimsingi wala hazileti fikirishi kwa mtu yeyote anayejua maana
bunge ni nini, na nani mwenye mamlaka na bunge!? Bunge ni mali ya umma, na umma ndiyo
unalichagua bunge na kama umma ndiyo unalichagua bunge sioni sababu ya kuwafungia
wabunge wasionekane au wasisikike wanachokiongea kwa kisingizio cha kukiuka maadili na
kanuni za bunge!
Tena ni vizuri wabunge wanapopigana wananchi waone ili wajue kinachowapiganisha ni kitu
gani? Kinachowapiganisha kinalenga maslahi ya umma au binafsi; wananchi wanataka kuona
ni mbunge gani yupo tayari kupigana na hata kung’olewa meno kwa ajili yao! Hivyo npyo
tunavyowapima wabunge wale wanaojitoa muhanga kwa ajili yetu, na pia kuwaona wale
wanafiki wakisimama majukwaani wanatoa ahadi za uongo kwamba watasimamia haki lakini
wakiingia bungeni ni waoga hata kunyosha kidole wanaogopa!
Wabunge kupigana bungeni ni jambo la kawaida kwa mabunge mengi duniani, tumewahi
kushuhudia wabunge wa Uingereza, Urusi, Ukraine, Marekani, Brazili na kwingineko wabunge
wakishindana kuhusu hoja na kuishia kurushiana matusi na mwishowe kupigana, hivyo na sisi
tusione kitu cha ajabu wabunge kupigana, kwa vile kupigana kwa wabunge ni ishara ya kukua
kwa democrasia. Ukikuta bungeni hakuna mizozo wala mivutano ya hoja, basi jua kwamba
hakuna democrasia na bunge hilo ni bunge la mwelekeo mmoja.
Sababu alizotoa katibu wa bunge Dr. Thomas Kashililah za kwamba wabunge wanawake
wanapojua kwamba watatoa hoja, huwa wanakuja wamevaa vizuri na kujipodoa akiitumia
sababu hii kama kigezo cha kutorusha matangazo moja kwa moja; mimi naoni hii ni sababu
isiyokuwa na msingi kwa vile mwanamke hata akienda gengeni kununua nyanya ni lazima
ajipodoe! Sasa unataka akiingia bungeni awe amevaa ovyo ovyo wakati anaenda kusikilizwa na
waajiri wake ambao ni wananchi! Wakimuona amevaa ovyo ovyo na hakujipodoa si wananchi
watamnyima kura uchaguzi ujao!?
Dr. Thomas Kashililah anaposema baadhi ya wabunge wanapochangia hoja huwa
wanazungumza mpaka mishipa inatoka, hivyo anataka kuitumia hoja hii kama sababu ya vikao
vya bunge kutorushwa moja kwa moja; pia hii si sababu ya msingi ambayo inaweza kutolewa
na katibu wa bunge; bungeni ndipo sehemu pekee ya kuonyesha umahiri wa kuongea kwa vile
bungeni ni jukwaa pekee linalotambuliwa kikatiba katika kutetea maslahi ya umma; na kama
mbunge atalitumia jukwaa hili kwa manufaa yake wewe muache tu kwa vile sisi wananchi
tupo macho tunamuangali moja kwa moja kupitia runinga zetu. Akizidisha umimi 2015
tutampumzisha!
Dr. Thomas Kashililah anaposema waandishi wa habari wanampiga picha spika akiwa ameinama
au amelala bungeni, na akitaka kukitumia kigezo hichoi kama kuunyima umma wa watanzania
kutoshuhudia bunge lao ambalo wameliajiri na kuliruhusu kutumia kodi zao, pia ni sababu
ambayo haina msingi na kulingana wadhifa aliokuwa nao katibu wa bunge hakustahili kutetea
sababu kama hiyo, kwa vile bungeni ni jukwaa la kujadili matatizo ya wananchi na wala siyo
sehemu ya kulala au kupumzika; kama spika analalalala bungeni inaoshesha hatekelezi wajibu
wake kikamilifu na kama ndiyo hivyo ni kwanini bunge lisimuwajibishe!?
Bwana Kasililah anataka aturejeshe nyuma kwenye zile enzi za giza la kikomunist ambapo
wabunge walikuwa wanajifungia na kuongea mambo waliyotaka na baada kuyachambua yale
tuliyostahili kuyasikia na kutangaziwa kwa njia ya redio, na yale tusiyostahili walibaki nayo
wenyewe! Bunge la kikomunist hupangiwa uvae nguo gani!? uulize swali gani!? utoe jibu
gani!? mwandishi wa habari apige picha gani au akaandike kwenye gazeti kitu gani!? Huu ndiyo
utaratibu wa mabunge ya kikomunist yalivyokuwa enzi hizo, sasa wewe na uelewa wako unataka
uwarudishe watu kizani kwa maslahi yako binafsi, hatutakubali kwa hilo hata siku moja. Wewe
waache wabunge wafanye wafanyavyo sisi ndiyo waajiri wao ukifika muda wa kusitisha ajira
zao tutafanya hivyo mara moja, wewe tunachokuomba ukiona spika amelala na huku bunge
linaendelea mwamshe ili azinduke usingizini asije akaidhinisha sheria za maangamizi!
Dr. Noordin Jella (Ph.D. in Economics)
Former Lecturer of Mzumbe, Open & KIU – Dar, Universities.
Currently: Freelance Journalist & Seasonal Political
Analyst
Email: norjella@yahoo.com
Mobile: +255 782 000 131

No comments:

Post a Comment