
Ndugu zangu,
Juzi hapa nilikuwa nafatuna karanga
Kwa mwanadamu, suala si kutafuna karanga tu, bali, umuhimu wa kujua kitakachotokea kwa karanga ya mwisho. Maana, unaweza kutafuna karanga tamu, lakini, karanga ya mwisho ikiwa imeoza, basi, itaharibu utamu wa karanga zote ulizotangulia kuzitafuna.
Hivyo, ni heri karanga mbovu iwe ya kwanza kutafunwa, kama utapata bahati mbaya hiyo.
Swali; Je karanga ya mwisho ikiwa tamu sana itakuwaje?
Jibu; hilo ni jambo la kheri, maana, hata hapo katikakati ukiwa umetafuna karanga mbovu, karanga ya mwisho itafuta machungu ya karanga mbovu ulizotafuna.
Na kwa mwanadamu karanga ya mwisho ikiwa tamu sana, basi, usiwe na tamaa ya kutafuna karanga nyingine. Utaambulia zenye mang'onying'onyi. Na hutakuwa tena na hamu ya kuonja karanga!
Naam, tafakari karanga yako ya mwisho!
Na hilo ni Neno la Leo.
Maggid Mjengwa,
Dar es Salaam
0788 111 765
No comments:
Post a Comment