WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Saturday, April 19, 2014

Tanzania kwanza walaani Ukawa kususa


Dodoma. Kundi la Tanzania Kwanza linaloundwa na baadhi ya wajumbe wa Bunge la Katiba limelaani hatua ya kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwa kususia vikao vya Bunge hilo linaloendelea mjini hapa.

Mwenyekiti wa Tanzania kwanza Said Nkumba akizungumza na waandishi wa habari jana alisema, kundi lake linakichukulia kitendo cha Ukawa kama usaliti ili kuwapotezea matumaini wananchi ya kupatikana kwa Katiba Mpya kama ilivyokusudiwa.

“Tunachukulia kama usaliti kwa wananchi ambao wana matumaini ya kupata Katiba itakayopendekezwa na itakayolenga kuwaondolea kero za maisha hivyo kuwawekea misingi imara ya maendeleo,” alisema Nkumba.

Alisisitiza, “Kwa kitendo hiki, Tanzania Kwanza tunawaambia wananchi hawa Ukawa hawana nia njema wala uchungu na nchi hii na kwani sababu wamekimbia na kuacha nafasi ya kuwatetea wanawake, watoto na watu wenye ulemavu, vijana na wazee pamoja na makundi mbalimbali ya kijamii,” alisema.

Nkumba alisema kundi la Tanzania Kwanza linawatoa hofu wananchi kwa kuwa mchakato utaendelea kwa kushirikiana na wale wenye uchungu na wanaotambua wajibu wao katika kulienzi taifa kwa kuhakikisha wanafanikisha lengo lililokusudiwa.

Alisema Ukawa walionyesha nia ya kukwamisha mchakato huo kwa visingizio mbalimbali ikiwamo la kubishana kuhusu upigaji wa kura wakitaka kura za siri lakini waliporuhusiwa kupiga za siri na wazi wakaanza kuwalazimisha wajumbe wao kupiga kura za wazi.

source: mwananchi

No comments:

Post a Comment