WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, April 15, 2014

Ikulu yaweka hadharani hati halisi ya Muungano

Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue.
Ikulu  imeweka hadharani hati ya makubaliano ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, iliyotiwa saini na waasisi, hayati Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume Aprili 22, 1964.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, aliwaambia waandishi wa habari Ikulu, jijini Dar es Salaam jana kuwa wakati wowote kama Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta, ataiomba hati hiyo ipelekwe bungeni kujadiliwa au kuwekwa wazi, Ikulu italikubali ombi hilo.

Alitaja sababu za hati hiyo kutoweka hadharani hadi kuhojiwa, kuwa ni unyeti wake kwa nchi.

"Utaandaliwa utaratibu wa hati hiyo kuwekwa kwenye Makumbusho ya Taifa ili kila mwananchi waione," alisema Balozi Sefue.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema jana kuwa Ikulu imemtumia faksi ya hati hiyo na kwamba, amekwishakuikabidhi kwa ofisi ya Mwenyekiti wa Bunge hilo.

Naye Sitta alisema hati hiyo itatolewa nakala na kila mjumbe atapewa hati iliyosainiwa na kupelekwa bungeni.

 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment