WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Wednesday, April 16, 2014

Mamia wajitokeza kumzika Gurumo


Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza la aliyekuwa nguli wa muziki wa dansi nchini, Muhidin Maalim Gurumo kwenda makaburini katika Kijiji cha Masaki, Kisarawe mkoani Pwani jana. Picha na Venance
Pwani. Safari ya miaka 74 duniani ya nguli wa muziki wa dansi nchini, Muhidin Mwalimu Gurumo ilifikia tamati jana baada ya kuzikwa kijijini kwake Masaki Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani.
Gurumo alifikwa na mauti Aprili 14, mwaka huu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa amelazwa kwa matibabu ya ugonjwa wa moyo, maradhi yaliyomsumbua kwa kipindi kirefu.
Safari ya mwisho ya nguli huyo ilianzia jana asubuhi nyumbani kwake Tabata External kwa waombolezaji wakiongozwa na Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal kutoa heshima za mwisho na salamu kutoka makundi mbalimbali kutolewa.
Msafara wa magari zaidi ya 20 ulianza saa 05:15 kwenda Masaki na ulifika saa 7:10 nyumbani kwake. Mwili wa Gurumo ulipelekwa msikitini kwa ajili ya sala kisha saa 07:40 mazishi yalifanyika katika makaburi ya Masaki mkabala na ilipo nyumba yake.

Akimzungumzia nguli huyo wa muziki, mtangazaji mkongwe ndani na nje ya nchi, Tido Mhando alisema tungo za nyimbo alizoimba Gurumo zilikuwa zenye kuelimisha na  kuiburudisha jamii.

Mhando, ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya  Mwananchi Communications Limited (MCL), alisema Gurumo  alitumia tungo zake kuhamasisha jamii na kupigania uhuru wa  Waafrika.
“Jana (juzi) kuna redio ilikuwa ikipiga nyimbo zake zaidi ya 20. Hakika nyimbo zote zilikuwa nzuri kutokana na umahiri wake wa utunzi vitu, ambavyo vijana wetu wanashindwa kufanya hivyo leo hii,” alisema Mhando.

Aliongeza: “Vijana wetu wanatakiwa kuiga kutokana na ustadi wa Gurumo wa kuimba, ustadi wa lugha ya Kiswahili, hivyo waige mfano wake.”

source: mwananchi

No comments:

Post a Comment