WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Wednesday, April 16, 2014

Okwi,Kaseja wafungiwa vioo Yanga

Katibu Mkuu wa Yanga,Beno Njovu.
Wachezaji Emmanuel Okwi na Juma Kaseja wameenguliwa kwenye kikosi cha Yanga kitakachoikabili Simba katika mechi yao ya kukamilisha ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Simba Jumamosi, uongozi wa klabu hiyo ya Jangwani ulisema jana.
Kwa mujibu wa kocha msaidizi wa Yanga, Boniface Mkwasa, wachezaji hao wa zamani wa klabu ya Simba, hawatacheza dhidi ya timu hiyo kutokana na kukosekana mazoezini na wenzao na suala lao liko chini ya uongozi.

Mkwasa alisema timu yao ina kikosi kipana hivyo haitambembeleza mchezaji yeyote acheze na akasisitiza kwamba kila mmoja anapaswa kuheshimu misingi ya mkataba wake.
"Uongozi unajua hatua stahiki za kuchukuliwa dhidi yao," alisema Mkwasa ambaye pamoja na kocha mkuu wake Mholanzi Hans van der Pluijm waliingia madarakani katika mzunguko wa pili wa ligi wakichukua mikoba ya Mholanzi Ernie Brandts na msaidizi wake Fred Minziro.
Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu, hakupokea simu yake jana kuzungumzia hatua watakazochukua dhidi ya wachezaji hao, huku pia Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto akisema yuko nje ya ofisi na simu ya Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga pia ikiwa haipatikani. 

Mkwasa alisema timu yao haitakubali kufungwa kirahisi na Simba mara hii kama ilipokubali kipigo cha 3-1 katika mechi yao iliyopita ya kirafiki ya Nani Mtani Jembe.

Kuhusu mechi hiyo, winga wa Yanga, Simon Msuva, ametamba kuwa timu yao itaibuka na ushindi mnono kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumamosi.

UCHAGUZI MKUU JUNI 15

Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam itapata viongozi wapya Juni 15 mwaka huu, imeelezwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana katika mtandao wa klabu hiyo, kikao cha Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo kilichoketi Aprili 10 kiliazimia mkutano mkuu wa uchaguzi ufanyike siku hiyo..

Taarifa hiyo ilieleza kuwa taratibu za uchaguzi zitatangazwa baadaye na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Alex Mgongolwa.

Akizungumza na NIPASHE juzi akiwa Moshi, Kilimanjaro ambako Yanga juzi ilipiga kambi ikitokea Arusha, Msuva alisema anaamini Yanga italipa kisasi cha kufungwa 3-1 dhidi ya Simba na kusababisha kutimuliwa kwa benchi zima la ufundi la Yanga lililokuwa likiongozwa na Mholanzi Ernie Brandts.

"Tunashukuru Mungu tumeshinda mechi ngumu ya Arusha licha ya ubingwa kwenda kwa Azam lakini tuna kazi nyingine ya kuhakikisha tunaifunga Simba mechi ya mwisho. Sioni kitakachotukwamisha tena kuifunga Simba," alisema winga huyo aliye katika kiwango cha juu.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment