WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Sunday, January 20, 2013

YANGA YAFANYA MKUTANO MKUU WA WANACHAMA SALAMA



Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuf Manji (katikati) akielezea jambo mbele ya wanachama waliohudhuria mkutano mkuu leo katika Ukumbi wa bwalo la Polisi - Oysterbay , Lawrence Mwalusako katibu mkuu (kushoto) na Clement Sanga makamu mwenyekiti (kulia)

Klabu ya Young Africans Sports Club leo imefanya mkutano mkuu wa mwaka wa wanachama katika Ukumbi wa Bwalo la Polisi eneo la Oysterbay, huku mkutano huo ukiendeshwa kisasa kwa kuonyeshwa moja kwa moja (live) na kituo cha Luninga cha Clouds nchini kote.
Mkutano ulianza majira ya saa 5 kasoro, huku wanachama wakijitokeza kwa wingi katika mkutano huo ambao ulikuwa haujafanyika kwa kipindi kirefu katika Klabu ya Yanga.

Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuf Manji alifugua mkutano kisha makamu mwenyekiti aliongoza sara kwa upande wa wakristo na mzee Ibrahim Akilimali alisoma dua kwa upande wa dini ya Kiisalamu.

Katika mkutano huo wanachama wameridhia kuongezewa muda wajumbe wa Bodi ya Wadhamini, Mama Fatma Karume na Francis Kifukwe huku wanachama wakipitisha majina ya Captain George Mkuchika na Balozi Ameir Mpumbwe kuwa wajumbe wa Bodi ya Wadhamini.

Uongozi unaandaa taratibu nzuri kwa kadi za uanachama na kwa sasa wapo katika maongezi na baadhi ya taasisi za fedha ili waweze kufanya hivyo, pia katiba inabidi iboreshwe na mkutano mkuu wa wanachama uwe kila baada ya miezi sita (6) badala ya miezi mitatu (3) yahivi sasa.

Ifuatayo ni vipengele ambavyo wanachama wamevipisha katika mkutano wa leo;

Katiba - Uchaguzi mgombea nafasi ya mwenyekiti awe namgombea mwenza ili wapate fursa ya kutekeleza mipango/malengo kwa pamoja, tofauti na sasa ambapo kila mgombea anakuwa na mawazo na malengo yake.

Pia Mwenyekiti na makamu mwenyekiti watakua na fursa ya kuchagua wajumbe wa kamati ya utendaji kulingana na mahitaji ya kipindi hicho.

Ujenzi wa Uwanja - Kamati ya utendaji inaendelea na mchakato wa kutafuta njia ya kuweza kupata pesa ya kujenga uwanja na eneo la mafia

Mkadirio ya uwanja ni bl 32, ambapo uwanja utakua na uwezo wa kubeba watu elfu arobaini (40,000) ukiwa na eneo la kuegeshea magari na huduma zote za muhimu katika viwanja vya michezo.

Makamu mwenyekiti alipata fursa ya kuwaonyesha wanachama ramani na michoro ya uwanja mpya unaontarajiwa kuanza ujenzi wake mwishoni mwa mwezi wa tano mwaka huu, ambapo uwanja unatazamiwa kujengwa kwa kipindi cha miaka miwili na kampuni ya ujenzi ya BCCG iliyojenga uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Aidha katika mkutano huo Mwesigwa Selestine, Lousi Sendeu na Godwin Muganyizi wamefutiwa uanachama baada ya kuwa wamefungua kesi za madai dhidi ya klabu yao ya Young Africans. 

Manji alisema pia kuahitajika maboresho katika baadhi ya mikataba kama ya TBL, Push Mobile, Pecha (kalenda) na vifaa vya Yanga (jezi,kofia,kalamu,skafu,suaruali za mazoezi nk) ili viweze kuisadia klabu kuweza kujiendesha kulingana na kipato kinachopatikana.

Katika kitengo cha fedha kuna madeni ambayo Yanga inadaiwa na uongozi bado unahitaji kuyafuatilia ili kuweza kujua uhalali wa madeni hayo:

(i)Cross Road - U$1600 (gharama ya ndege kutoka Zambia)

(ii)Holiday Dreamer - U$ 5079 (gharama za ndege kwenda Cairo) 

(iii)Mwesigwa Selestine - milioni 183.4

(iv)Louis Sendeu - milioni 79 

Pia kuna fedha ambazo zimetumika bila ya idhini ya kamati ya utendaji millioni 288 hazina maelezo, milioni 85.6 bila ya idhini ya kamati ya utendaji na milioni 8.6 hazina ushaidi wa matumizi. 

Mwisho Uongozi uliweza kutoa vyeti vya utambuzi kwa baadhi ya wanachama na wachezaji/viongozi kwa mchango wao katika Klabu ya Yanga, waliopewa vyeti hivyo ni:

1.Abdallah Bin Kleb - kongozi anayejitolea sana katika kuhakikisha timu inafanya vizuri na kushinda michezo inayoikabili

2.Shadrack Nsajigwa - mchezaji aliyechezea Yanga kwa muda mrefu (barua na fedha taslimu tsh 1,000,000/=) 

3.Mahmoud Momar - (mtunza vifaa) mfanyakazi wa siku nyingi katika benchi la ufundi (barua na fedha taslimu tsh 1,000,000/=)

4.Stephen Samuel - mwanachama bora na mwenye uchungu na timu ya Yanga (barua na zawadi ya pikipiki mpya)

5.Hayati Isamail Rashid - mwanachama aliyesaidia kupatikana kwa muafaka (barua)

Mwisho mwenyekiti alifunga mkutano kwa kuwashukuru wanachama wote waliojitokeza katika mkutano huo wa leo, ambapo wanachama waliouhudhuria mkutano ni 1440 huku mkutano ukiendeshwa kwa masaa matatu tu (live) moja kwa moja na kituo cha runinga cha Clouds Tv ambayo kupitia kampuni yake ya Prime Time Promotions ndio walikuwa waandaji wa mkutano huo.


 Wanachama wa timu ya Yanga kutoka sehemu mbalimbali wakitawanyika nje ya jengo la bwalo la Maofisa wa Polisi,Oysterbay jijini Dar mapema leo mchana mara baada ya kumalizika mkutano wao mkuu wa Mwaka,ambao kwa hakika umefanikiwa kwa kiasi kikubwa,Mkutano huo uliratibiwa na kampuni ya Prime Time Promotions Ltd ya jijini Dar na kurushwa Live kupitia Clouds TV,aidha Mkutano huo ulionekana kunoga zaidi kufuatia timu hiyo ya Yanga kuifumua timu ya Black Leopards ya nchini Afrika kusini  katika mechi yao ya kirafiki iliyofanyika hapo jana kwenye Uwanja wa Taifa bao 3-2.

 Mwenyekiti Mpya wa Club ya Yanga Africans,Yusuf Manji akifafanua mambo mbalimbali kwenye mkutano huo,uliochanganua mambo mbalimbali zikiwemo changamoto za timu hiyo,maendeleo yao mbalimbali ikiwemo samabamba na ujenzi wa kiwanja kikubwa cha mpira maeneo ya Jangwani,jijini dar,Sahihisho la katiba yao,masuala mbalimbali ya yanayohusiana na wanachama wao,ustawi wa wanachama wao,mikataba baina yao na wadhamini wao na mambo mengine mbalimbali.
 Sehemu ya meza kuu ya mkutano huo ilivyokuwa.
 Makamu mwenyekiti wa timu ya Yanga,Clement Sanga akitolea ufafanuzi moja ya jambo lililoulizwa na wajumbe wa mkutano huo.
Pichani kulia ni mchezaji wa timu ya Yanga,Shadrack Nsajigwa akipeana mkono wa shukurani na Mwenyekiti wa Yanga,Yusuf Manji mara baada ya kutajwa kuwa ndiye mchezaji aliyedumu Yanga kwa muda mrefu miongoni mwa wachezaji waliopo hivi sasa,hivyo alizawadiwa barua ya shukurani na kitita cha shilingi milioni moja.
Pichani juu na chini ni baadhi ya Wajumbe wa timu ya Yanga waliopata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali kwa Kamati ya Utendaji,mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Yanga,Yusuf Manji sambamba na Makamu mwenyekiti wa timu hiyo,Clement Sanga wakifatilia jambo kwa  makini ukumbini humo.
 Pichani baadhi ya wachezaji wa timu ya Yanga pia walihudhuria mkutano huo uliohusu mikakati mbalimbali ya kuimarisha timu hiyo.
 Baadhi ya Wazee wa baraza wa timu ya Yanga wakifautilia kwa makini yaliyokuwa yakijili kwenye mkutano huo mkuu wa Kihistoria.
 Kocha mpya wa timu ya Yanga,kutoka nchini Uholanzi Ernest Brandts nae aliruhusiwa kutoa yake machache kuhusina na timu yake ya Yanga.
 Pichani ni baadhi ya Wanachama wa Yanga waliofurika kwa wingi ndani ya mkutano mkuu wa timu hiyo uliofanyika ndani ya bwalo la Maofisa wa Polisi,Oysterbay jijini Dar es salaam mapema leo asubuhi na kumalizika mapema jioni ya leo. 
 Msanii mahiri wa kizazi kipya sambamba na wasanii wenzake kutoka THT wakitumbuiza kwenye mkutano huo.
Mtangazaji machachari wa kipindi cha michezo,Clouds FM/TV Mbwiga Mbwiguke akiwaweka sawa wanachama wa Yanga waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wao mkuu wa Mwaka.Picha Kwa Hisani ya Full Shangwe Blog na  vijimambo blog

No comments:

Post a Comment