WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Sunday, January 27, 2013

VURUGU ZINAZOENDELEA MTWARA






Jengo la Mahakama lilochomwa moto
Chumba cha Jenereta kilichochomwa moto
Nyumba inayosemekani ni nyumba ya waziri ikiwa imeharibiwa vibaya
Nyumba inayosemekana ni ya Mwenyekiti wa CCM
 
Magari 18,Pikipiki 7 vyateketezwa kwa moto kwa moto vyote vikiwa ni mali za Halmashauri ya masasi na baadhi ni vya watumishi wa halmashauri
Gari la Wagonjwa likiteketea kwa moto

Sehemu ya magari yakiendelea kuteketea kwa moto.Picha Zote na Siraji Nalikame
----
Na  Said Powa

CHANZO cha vurugu za jana Mkoani Mtwara imeelezwa kuwa ni askari wa wanazinguka mjini na pikipiki maarufu kwa jina la Tigo kumkamata dereva wa pikipiki mmoja na kuanza kumpiga. Madereva hao walipoona tukio hilo la mwenzao kupigwa waliingilia kati mzozo huo na kumtoa mwenzao kwenye kadhia hiyo. 

 Baada ya kumtoa mwenzao kundi la madereva hao wa bodaboda waliandamana hadi kituo cha Polisi wilaya kwenda kueleza hisia zao lakini walipofika tu polisi walianza kufyatua mabomi yalio ibua hasira za wananchi na kuanza kusogelea ene la kituo hicho badala ya kukimbia.

Wananchi hao walijazana kwenye kituo hicho huku polisi wakiendelea kupiga mabomu lakini walionekana kushindwa wananchi haowakapata nguvu na kuanza kuchoma moto magari ya halmashauri na majengo.

Wakatoka hapo wakaenda kwenye nyumba ya Mbunge wa jimbo hilo wakaichoma moto wakaenda kwenye ofisi ya serikali ya mtaa, kwenye tawi la chama cha mapinduzi na baadaye kwenda kwenye nyumba ya Mwenyekiti wa bodi ya Korosho Mama Anna Abdalla.

Kwamujibu wa mmoja wa wananchi wa Masasi aliyejitambulisha kwa jina la Mussa amesema ameona magari manne yakiwa na majeruhi wa tukio hilo wakikimbizwa kwenye Hospitali ya Ndanda.

Aidha Mganga mmoja wa Hospitali ya Wilaya akizungumza na kituo kimoja Cha Radio alisema kuwa hospitalini hapo wamepokea miili ya watu watatu lakini amesema kuna uwezekano mkubwa idadi ya watu waliokufa ikawa kubwa zaidi kwasababu wapo wengine wamechukuliwa na nduguzao hukohuko kwenye matukio.-
-

Mtiririko wa taarifa mpya (updates) kutoka kwa Baraka Mfunguo
  1. NEWALA: Nyumba ya Mkuchika inawaka moto -- Taarifa za redio mbao sasa  ni kwamba wananchi wanaendelea kufanya uharibifu mkubwa huko ambapo naambiwa wamevamia gereza wakafungulia wafungwa na kisha kupiga moto gereza. Polisi wamezidiwa na wamejifungia kituoni wanarusha mabomu yao tokea huko walikojificha maana nje hakutamaniki. Na wameshateketeza nyumba ya mama Anna Abdallah.
  2. Kikao cha dharura cha kamati ya ulinzi na usalama kinaendelea kwa kuwashirikisha maafisa wa polisi na maafisa usalama waliotoka Dar es Salaam kuongezea nguvu.
  3. Maaskari na makachero wawasili  Mtwara leo asubuhi na helkopta kuongezea nguvu.
  4. Hosteli ya wanafunzi wa chuo cha Utumishi maeneo ya Kiyangu B Mtwara yakoswa koswa kuchomwa moto kwa kile kinachodhaniwa kuwa na uhusiano na Hawa Ghasia mpaka sasa wanafunzi hawana mahala pa kukaa.  Kituo kidogo cha Polisi Cha Shangani mkoani Mtwara nacho chakoswa na moto. Ofisi ya Afisa Mtendaji Nkanaledi mkoani Mtwara nayo yavunjwa.
  5. Wananchi wamechoma moto mahakama ya Mwanzo na kuvunja vioo vya nyumba za waheshimiwa Hawa Ghasia (Waziri, TAMISEMI) na ya Mohamed Sinani (Mwenyekiti wa CCM Mkoa) zilizopo mtaa wa Sinani.
  6. Wakiwa katika mahakama ya mwanzo, Polisi walizingirwa na vijana waliokuwa wamebeba mawe na kufunga barabara zote za kuingia na kutoka Kituo Kikuu cha Mabasi na eneo la Soko Kuu, licha ya kufyatua hewani mabomu ya machozi. 
  7. Baadhi ya barabara za zimezibwa kwa kuchomwa matairi ya gari, na kuongeza hofu kwa wananchi.
  8. Hali imeshakuwa mbaya masasi taarifa zilizotufikia punde wamechoma eneo linaloitwa loliondo, ofisi za elimu na ofisi ya trafiki, inasemekana jamaa wameshavamia ofisi za halmashauri wengine wako njiani nyumbani kwa mama Ana Abdala, hapa Mtwara  mjini maduka yote eneo la soko kuu na stendi yamefungwa hakuna huduma, huko Newala , leo kuna mkutano mkubwa mchana huu wa kumkataa George Mkuchika.
  9. Vurugu zahamia wilaya ya Masasi mkoani Mtwara Nyumba ya Mbunge wa Masasi nayo yateketezwa kwa Moto hivi sasa...Madereva Bodaboda waandamana ...Vurugu zashamiri Mabomu kibao..Hali ni tete
----------------------------------------------

Kwa kile kinachoaminika kuwa ni kukua kwa MGOGORO WA GESI Mkoani Mtwara na Kusini kwa ujumla, usiku wa kuamkia leo Mahakama ya Mwanzo katika Manispaa ya Mtwara Mikindani imeteketezwa kwa moto huku nyumba ya Mbunge Hawa Gasia ikivunjwa vioo na kuchomwa motto wakati ile ya Mwenyekiti wa CCM Mtwara, ndugu Sinani ikiwa imevunjwa tu vioo.

Chanzo hasa cha vurugu hizo haziko wazi lakini wengi wanazihusisha na sakata la GESI kwani Hawa Gasia na Sinani wamekuwa kwa Muda Mrefu wakishutumiwa kwa kuchochea na kuridhia usafirishaji wa gesi hiyo kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam. Uchomaji huo wa moto uliambatana na vurugu na ulipuaji wa mabomu ya machozi kutoka kwa polisi na hadi wakafanikiwa kuzima jaribio la uchomaji wa Kituo cha Polisi cha Shangani.

Wakati huohuo kuna taarifa kutoka Masasi zikieleza nako kuibuka tukio la chomachoma mchana huu wa leo ikihusisha uchomwaji wa Offisi za Serikali, Polisi, nyumba za Wabunge na Offisi za CCM. Hali ya Masasi inaelezwa kuwa ni tete zaidi kuliko ilivyokuwa hapa Mtwara Mjini usiku wa jana ingawaje napo palikuwa na kimuhemuhe cha mabomu ya machozi kutoka kwa polisi.

Bado mpaka sasa haileweki ni nini hasa hatma ya mgogoro huu, maana kwa upande wake Serikali inaonekana kushikilia msimamo wake uleule wa kutaka kusafirisha gesi hiyo wakati upande wa raia wakiwa na msimao wao wa GESI KWANZA MAISHA BAADAYE, kwa maana kutoridhia usafirishaji wa gesi hiyo ikiwa ghafi kupelekwa Dar es salaam.

Wito wangu kwa Serikali ni kuwa, muda ni huu wa kukaa na wananchi ili kujadiliana juu ya mstakabali mzima wa tatizo hili na kutafuta suluhu. Muda ni huu kwa sababu si vyema kuacha hali iendelee kuharibika ndipo tuje baadaye tulazimike kuunda tume za watu kuchunguzwa. Si vibaya kwa Serikali kukiri au kurudi kwa raia na kusema pale ilipoteleza na kutafuta ni namna gani na ni njia ipi sahihi ya kuliendea suala hili.

Ewe Mungu! Ibariki Tanzania, Wabariki Watanzania.

Hassani Samli,
Mtwara.
+255717340671

SOURCE HAKI NGOWI BLOG

No comments:

Post a Comment