WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Monday, January 21, 2013

WANADMV WAMUAGA BALOZI, WENGINE WABUBUJIKWA NA MACHOZI


Picha Juu na chini Mhe. Mwananidi Sinare Maajar, Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico anayemaliza muda wake akiwa ameongozana na Rais ya Jumuiya ya Watanzania DMV, Bwn. Idd Sandaly huku akifuatiwa na Bwn. Shariff Maajar, mume wa Mhe. Balozi, wote kwa pamoja wakiingia ukumbini siku ya Jumapili Janauary 20, 2013, College Park kwenye sherehe ya kumuaga iliyoandliwa na Jumuiya ya Watanzania DMV.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico anayemaliza muda wake, Mhe. Mwanaidi Maajar akiongea machache kuwashukuru wanaDMV na Watanzania wote waishio nchini Marekani kwa kumkarimu na kuwa nae karibu muda wote alipokua Balozi wa Tanzania hapa Marekani, kulikofanya kazi yake kuwa rahisi, kuliko mjengea jina na baadhi ya wanaDMV waliopata nafasi ya kuongea machache kwa kumtakia Balozi safari njema, wengi wao walishindwa kujizuia walikua wakilengwa na machozi.
kutoka kushoto ni Muweka hazina Jumuiya ya Watanzania DMV, Bwn. Malasy, Mama Lily Munanka, mkuu wa Utawala na fedha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Bwn. Shariff Maajar, mume wa Mhe. Balozi, Mhe. Mwananidi Maajar, Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico anayemaliza muda wake, Bwn. Idd Sandaly, Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Raymond Abraham, makamu wa Rais Jumuiya ya Watanzania DMV na Amos Cherehani, katibu wa Jumuiya ya Watanznia DMV.
Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania DMV wakimzawadia Mhe. Balozi zawadi yenye maneno yanayomuhusu Mhe. Manaidi Maajar, pichani Balozi anaonekana akiyasoma maneno hayo
Mhe. Balozi akiionyesha zawadi aliyopewa na Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania DMV.
Mhe. Mwananidi Maajar Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico anayemaliza muda wake akiwa ameshika moja ya zawadi alizopewa na Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania DMV, wengine kwenye picha ni Bwn. Shariff Maajar (kushoto) mume wa Mhe. Balozi, Bwn. Idd Sandaly (watatu toka kulia) Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Bwn. Raymond Abraham (wapili toka kulia) Makamu wa Rais Jumuiya ya Watanzania DMV na Bwn. Amos Cherehani, Katibu Jumuiya ya Watanzania DMV.
Dj Luke kwa niaba ya Bloggers wa DMV akiongea machache kumshukuru Mhe. Balozi kwa kuwa karibu na wanahabari hao pia Dj Luke alimshukuru Balozi kwa kukubali kwake kuizindua Blog ya Vijimambo Oct, 23, 2010 na kuwepo kwake kwenye uzinduzi ule kumesaidia kwa kiasi kikubwa kuipaisha Blog hiyo. Vijimambo na timu yake wamemzawadia Mhe. Balozi kuweka tangazo la kampuni yake bila malipo kwa muda wa  mwaka mmoja.
Uongozi wa Jumuiya wakipata picha na Mhe. Mwanaidi Maajar na mume wake, Bwn. Shariff Maajar
Bodi ya udhamini pamoja na wajumbe kamati mbalimbali Jumuiya ya Watanzania DMV wakifuatilia jambo wakati Mhe. Balozi (hayupo pichani) alipokua akionga machache.
WanzaDMV wakimsikiliza Balozi
Makamu wa Rais Jumuiya ya Watanzania DMV akiongea machache kuhuhu Brigedia Jenerali Maganga (hayupo pichani) mwambata wa jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani anayemaliza muda wake.
Asha Nyang'aji (kulia) akimkabidhi Brigedia Jenerali Maganga na mkewe Love Maganga zawadi ya kumbukumbu kama shukurani ya mahusiano mazuri na wanajumuiya DMV aliyopewa na  Uongozi wa Jumuiya DMV
kwa picha zaidi bofya raed more






source vijimambo blog

No comments:

Post a Comment