WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Friday, January 25, 2013

`Vurugu zililenga Z'bar isitawalike'


NA MWINYI SADALLAH

Vurugu zilizotokea Zanzibar zilikuwa na malengo ya kutaka nchi isitawalike kutokana na vitendo vya hujuma vilivyokuwa vikifanywa na wafuasi wa Uamsho visiwani humu.


Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud Mohamed, alipokuwa akijibu swali la Mwakilishi Mohammed Haji Khalid, katika Kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea Chukwani mjini hapa jana.

Waziri Aboud alisema vurugu hizo zilizotokea Oktoba na Novemba, mwaka jana, zilisababisha hasara kubwa na Jeshi la Polisi kulazimika kufanya operesheni ya kurejesha hali ya amani Zanzibar.

Hata hivyo, alisema Jeshi la Polisi halikunyanyasa au kudhalilisha raia katika kipindi hicho isipokuwa askari walikuwa wakifanya kazi kuwatawanya na kuwakamata vijana waliokuwa wakifanya vitendo vya uhalifu.

Waziri Aboud alivitaja vitendo hivyo kuwa ni kupora mali za watu, kupiga watu, kutisha watu, kuweka vizuizi barabarani na kutupa mawe kwa malengo ya kutaka nchi isitawalike.

Alisema vitendo hivyo viliwathiri kwa kiwango kikubwa wananchi kwa kushindwa kufanya kazi za kawaida za kujitafutia riziki.

Alisema Jeshi la Polisi Zanzibar ni chombo muhimu katika kulinda usalama wa raia na mali zao na muhimu kazi zao kuthaminiwa na wananchi.

Hata hivyo, alisema kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba ya Zanzibar, hakuna kifungu kinachotoa mamlaka kwa Jeshi la Polisi kunyanyasa au kudhalilisha raia wake.

“Katika kipindi hicho, Jeshi la Polisi halikuendesha vitendo vilivyodaiwa, bali iliendesha operesheni ya kutawanya na kukamata vijana waliokuwa wakifanya vitendo kinyume na sheria,” alisema.

Awali, Mwakilishi Mohammed Haji Khalid, alitaka sababu za Jeshi la Polisi kati ya Oktoba na Novemba, mwaka jana walifanya vitendo vya kuwanyanyasa na kuwadhalilisha raia wakati wajibu wao ni kulinda usalama wa raia na mali zao.

Katika vurugu hizo, askari mmoja wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), aliuawa kwa kupigwa mapanga pamoja na makanisa na baa kuchomwa moto.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment