WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Sunday, January 27, 2013

MZUNGUKO WA PILI WA LIGI KUU TANZANIA TEAM ZINAZOONGOZA LIGI HIYO ZATOA OVYO


Jerson Tegete wa tatu kulia mshambuliaji aliyewafunga Prisons mabao mawii
Young Africans leo imeendeleza wimbi lake la ushindi katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom baada ya kuichapa tmu ya Tanzania Prisosns kutoka mjini Mbeya jumla ya mabao 3-1, katika mchezo uliofanyika jioni hii katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Young Africans ambayo inaongoza ligi kwa kuwa na pointi 32 na mabao 28 ya kufunga, iliingia uwanjani kwa ajili ya kusaka pointi 3 muhimu ambazo imefanikiwa kuzipata.
Mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete, 'Mkali wa Uturuki', akishangilia bao lake la pili, huku kipa wa Tanzania Prisons, akishangaa akiwa chini baada ya kushindwa kuokoa mpira huo uliopigwa na mkali huyo wa Uturuki. katika dakika ya 82. ambapo bao la kwanza pia lilifungwa na mkali huyo na la pili lilifungwa na Mbuyu Twite. Hadi mwisho wa mchezo huo Yanga 3-Tanzania Prisons 1.
Simon Msuva, akipiga krosi, wakati wa mchezo huo wa fungua dimba ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara, mzunguko wa pili kwa upande wa timu hizo, uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.
Didier Kavimbangu, akijaribu kutupia, wakati wa mchezo huo, ambapo shuti hilo lilipaa juu ya goli.
Sehemu ya mashabiki wa Yanga, wakishangilia bao la tatu lililoizamisha Tanzania Prisons na kuvunja matumaini ya kusawazisha na kuwafanya wachezaji wa Prisons, kuanguka kila mara ambapo kila aliyekuwa akianguka alikuwa ameshikwa na msuli.
Oscar Joshua, akijaribu kumfinya mchezaji wa Prisons.
Mashabiki wa Yanga, wakishangilia bao la Mbuyu Twite.
Dkt. Steven Ulimboka, akijumuika na mashabiki wenzake wa Yanga jukwaani, wakati wa mchezo huo. 
Askari Polisi wakimbeba Mlemavu kumtoa nje baada ya mlemavu huyo kuonekana akikimbia huku akiwa hana nguo alipokuwa akijaribu kuingia katikati ya uwanja, alipoulizwa mlemavu huyo alisema kuwa alikuwa akielekea kumpngeza Mbuyu Twite, baada ya kuachia shuti kali lililomkuna vilivyo na kutinga wavuni.
Seleka la kumbeba lilianza hivi.......
Kikosi cha mholanzi Ernest Brandts kiliuanza mchezo kwa kasi, na kupata bao la kwanza dakika ya 11 kupitia kwa Jerson Tegete aliyemalizia pasi safi ya kiungo mshambuliaji Saimon Msuva.

Dakika sita baadae dakika ya 17, mshambuliaji wa Elias Maguli aliipatia Prisons bao la kusawazisha kufuatia uzembe wa walinzi wa Yanga kuzembea kumkaba mfungaji aliyekokota mpira toka upande wa pembeni mpaka alipofunga bao hilo.

Didier Kavumbagu alikosa mabao ya wazi dakika ya 7 na dakika 27 huku kiungo Nurdin Bakari akikosa pia bao la wazi dakika ya 38 ya mchezo.

Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza Young Africans 1-1 Prisons FC.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Yanga kuutawala mchezo hali iliyopelekea kujipatia bao la pili kupitia kwa mlinzi wa kulia Mbuyu Twite aliyemalizia mpira uliokolewa na walinzi wa Prisons kufuatia piga nikupige ya Nadir Haroub, na Saimon Msuvalangoni mwa lango la Prisons kabla ya mpira huo kumkuta Twite aliyeukwamisha wavuni.

Jerson Tegete aliendelea kuwa mwiba kwa timu ya Prisons baada ya kuipatia Young Africans bao la tatu dakika ya 66, akimalizia pasi safi ya kiungo Nurdin Bakari aliyetanguliziwa mpira na Hamis Kiiza na Nurdin kuwatoka walinzi wa Prisons kabla ya kumpasia Tegete aliyeukwamisha mpira wavuni bila ya ajizi.

Kama washambuliaji wa Young Africans wangekuwa makini Yanga ingeweza kuibuka na ushindi wa mabao mengi kwani Jerson Tegete alikosa bao la wazi baada ya kuwapinga chenga walinzi wote wa Prisons lakini umaliziaji wake haukuwa mzuri.

Mpaka mwisho wa mchezo Young Africans 3- 1 Prisons FC

Kiungo Frank Domayo aliugua ghafla na kuondolewa katika orodha ya wachezaji ya waliokuwa katika listi ya kuanza na nafasi yake ilichukuliwa na Nurdin Bakari, Domayo alijisikia kizunguzungu hali iliyompelekea daktari wa timu ya Yanga Dr Nassoro Matuzya kufukiria huenda akawa na malaria, baadaye Domayo alijisikia nafuu na kuutazama mchezo wote kwa dakika 90.

Kocha mkuu wa Yanga Ernest Brndts amesema anashukuru timu yake kupata kwa ushindi katika mchezo wa leo, kipindi cha kwanza wachezaji wangu hawakuwa makini na hawakuzingatia maaelekezo yangu , lakini wakati wa mapumziko niliwaeleza nini wanapaswa kukifanya na hatimaye timu ilibadilika na kuweza kutengeneza nafasi za kufunga mabao mawili japokuwa walikosa nafasi zingine za wazi 

Kambi yetu ya mafunzo nchini Uturuki imetusaidia sana, wachezaji wanacheza kwa kujiamin ila kuna mapungufu madogo madogo yalijitokeza katika mchezo wa leo, benchi la ufundi tumeyaona na tutayafanyia kazi katika michezo itakayofuata alisema "Brandts"


Young Africans: 1.Ally Mustapha 'Barthez', 2.Mbuyu Twite/Juma Abdul, 3.Oscar Joshua, 4.Nadir Haroub'Cannavaro', 5.Kelvin Yondani, 6.Athuman Idd 'Chuji', 7.Saimon Msuva, 8.Nurdin Bakari/David Luhende, 9.Didier Kavumbagu/Hamis Kiiza, 10.Jerson Tegete, 11.Haruna Niyonzima
source: vijimambo blog

No comments:

Post a Comment