WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Saturday, January 19, 2013

Mwakyembe ang'aka.. Bandarini hapatoshi!


NA BEATRICE SHAYO

Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe

Hujuma zaidi zinaendelea kuigubika  bandari ya Dar es Salaam,  hali  inayomfanya Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe , kuipa siku mbili Bodi na Menejimenti ya Mamlaka ya Bandari (TPA) kueleza sababu za kuondolewa  kipengele muhimu kwenye mkataba wa ujenzi wa mtambo wa kupakua mafuta ya meli  (SPM).

Alitoa amri hiyo  jana  alipozuri bandari hiyo akiongozana na Mawaziri Dk. William Mgimwa-Fedha , Dk Abdallah Kigoda- Viwanda na Biashara na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene.

Ilielezwa kuwa kuondolewa kipengele hicho kutailazimu TPA  kugharamia  Dola milioni 300 karibu sawa na Sh. bilioni 500 katika kipindi cha miaka miwili za  kukarabati mtambo huo.

Wakati Dk. Mwakyembe akitoa agizo hilo, TPA ilieleza kuwa ili kuboresha huduma za bandari zote , Mamlaka hiyo inahitaji kupatiwa mkopo wa Dola bilioni nne.

Baada ya  taarifa hiyo Waziri huyo alimbana Kaimu Mkurugenzi wa TPA, Madeni Kipande, akihoji kuwa wakati Mamlaka hiyo inakabidhiwa SPM, mzabuni   aliyeujenga mtambo huo kampuni ya Leighton ya Singapore alionyesha kuwa kipengele muhimu kimeondolewa katika mkataba huo.

Waziri  Mwakyembe alieleza zaidi kuwa  awali mkabata huo ulimtaka mzabuni huyo anapokamilisha kazi yake alitakiwa kuacha vifaa vya ukarabati wa mtambo huo  vyenye  thamani ya Dola milioni 300  (bilioni 500). 

“Nashangaa kampuni hii haikuacha vifaa hivyo kwanini na vifaa hivyo vingetumika kukarabati  kwa muda wa miaka miwili na pia tusingeingia gharama zozote sasa tunataka kujua aliyekichomoa kipengele hiki ni nani ili na sisi tumchomoe.” Alisema Dk Mwakyembe.

Baada ya Dk Mwakyembe kuzungumza hayo, Simbachawene alihoji tena kwa Kaimu Mkurugenzi  ni kwanini mkataba ubadilishwe wakati kipengele cha mkataba huo kilikuwa ni muhimu kwa  mwekezaji  huyo kupatiwa zabuni ya ujenzi wa mtambo huo? “Hivi  hapa TPA si kuna wanasheria, iweje litokee hili jambo”. alihoji Simbachawene

Kipande akijibu hoja hiyo alisema baada ya zabuni   kupita kipengele hicho kiliondolewa na kuifanya TPA kuingia gharama za kufanya matengenezo. Baada ya maelezo hayo , Dk. Mgimwa aliongeza kuwa serikali inahitaji kumfahamu aliyekiondoa kipengele hicho kwani jambo hilo linaonyesha TPA kuhujumiwa.

Aliitaka bodi ya TPA  kueleza  ilichukua hatua gani.
Baada ya  malumbana hayo Dk. Mwakyembe aliitaka Bodi na Menejimenti ya TPA kufanya kikao cha  Jumatatu ijayo na siku hiyo kumpekea maelezo ofisini kwake.
Alisema taarifa hiyo ataipeleka kwa mawaziri  aliokuwa ameongoza  nao ili  kutoa kauli ya pamoja.

Mbali na hilo Dk Mwakyembe pia alisema kuanzia sasa  kampuni  za kigeni na za ndani hazitapewa vibali  vya  kujenga bandari kavu za kuhifadhi shehena karibu na eneo la bandari kwani hazipunguzi mrundikano wa mizigo bandarini.

Katika hatua nyingine Dk Kigoda aliliagiza Shirika la Viwango  (TBS)  kufanya kazi kwa saa 24  bandarini humo.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment