WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Saturday, December 1, 2012

Mali Za Marehemu Sharo Milionea Zaanza Kurejeshwa




Baadhi ya vitu vya marehemu Sharo milionea vilivyokamatwa baada ya msako mkali baina ya Polisi na wananchi wa Kijiji Songa Kibaoni.
---
Na: Mashaka Mhando,Tanga
  
WATU wanaosadikiwa kuiba vitu vya marehemu Hussein Mkiety maarufu kwa jina la 'Sharo Milionea' aliyefariki kwa ajali ya gari katika kijiji cha Songa Kibaoni wilayani Muheza Novemba 26 mwaka huu, wamesalimisha baadhi ya vitu hivyo kwa mwenyekiti wa Kijiji hicho huku wakiendelea kuishi mafichoni kuogopa kutiwa mbaroni.

Watu hao wamesalimisha vitu hivyo baada ya Mkuu wa wilaya ya Muheza Subira Mgalu ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama kuwatangazia kwamba wale wote waliomwibia marehemu watasakwa na kuchukuliwa hatua za kisheria kufutia kitendo walichokifanya kutokuwa cha kiungwana.

Mkuu huyo pamoja na jeshi la polisi wilayani humo waliendesha msako juzi usiku lakini hawakuweza kuwakuta watu baada ya kuzihama nyumba zao kuogopa kutiwa mbaroni na mkuu huyo kuwalazimsha baadhi ya familia walizozikuta kuendesha zoezi la kuwataja watu wanaohofiwa kwamba huenda watakuwa wamchukua vitu hivyo.

Kamanda wa polisi mkoani Tanga ACP Constatine Masawe, aliwaeleza waandishi wa habari ofisini kwake kuwa, usiku wa kuamkia juzi mwenyekiti wa kijiji hicho Abdi Zawadi alipelekewa vifaa mbalimbali ikiwemo nguo ambazo marehemu alikuwa amezivaa pamoja na spea tairi ambalo waliling'oa na kutokomea porini.

Kamanda huyo alitaja vitu vilivyokabidhiwa kwa mwenyekiti huyo kuwa ni pamoja na begi lake lililokuwa na 'viwaro' nguo zake, betri ya gari hilo lililokuwa na namba T 478 BVR aina ya Toyota Harrier, saa yake ya mkononi, simu yake aina ya Blackberry na redio ya gari iliyokuwa pia imeng'olewa na wezi hao.

Kamanda huyo alisema vitu hivyo vilipelekwa na mtu mmoja ambaye kwasasa jeshi hilo linashindwa kumtaja jina lake kwa vile alijitambulisha kwamba ana undugu na wezi hao ambao walimpa vitu hivyo avipeleke kwa uongozi wa kijiji hicho hatua ambayo alidai kwamba wanafanya uchunguzi ili kuwatia nguvuni wale wote waliohusika na tukio hilo.
 
Alisema waliweka mtego baada ya kusikia kwamba kuna mwizi mmoja wapo anaitafutia mteja simu ya mkononi ya marehemu lakini wakati wameweka mtego huo kijana huyo alipokuwa akijadiliana bei na mtu waliyemweka, alibaini na alipompa mkononi alikimbia vichakani kuogopa kukamatwa.
 
Kamanda huyo aliwashukuru baadhi ya wananchi wa kijiji hicho pamoja na Mkuu wa wilaya kuhakikisha wanashirikiana na jeshi hilo ili kuwabaini na kuwakamata wote waliohusika katika tukio hilo ambalo limetokea huku wananchi kadhaa wakiomboleza kifo cha msanii huyo ambaye alizikwa kijijini kwao Lusanga wilayani Muheza juzi.

Katika hatua nyingine kamanda huyo alisema katika matukio ya ajali yaliyotokea mwezi huu wa Novemba jumla ya ajali 10 zilitokea ambazo zimesababisha vifo ni 7 na zilizosababisha watu kujeruhiwa ni tatu, kati ya hizo watu 12 walipoteza maisha na wengine wanane walijeruhiwa.

Kamanda Masawe alisema jumla ya makosa 2,365 yalitendeka na kupigwa faini iliyosababisha serikali kujiingiza kiasi cha sh. 70,950,000 hatua ambayo kamanda huyo alisema haioneshi kwamba watumiaji barabara wamekuwa wakifuata wakitii sheria za usalama barabarani.

1 comment:

  1. tabia chafu sana.iwe fundisho kwa watanzania wengine.kumkata vidole marehemu ni unyama.

    ReplyDelete