WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Wednesday, December 5, 2012

Maalim Seif aipongeza Zanzibar Heroes



Na Hassan Hamad OMKR

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ametuma salamu za pongezi kwa timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kwa kufanikiwa kuingia katika hatua ya nusu fainali kwenye michuano ya kombe la challenge.

 
Zanzibar Heroes imeingia hatua hiyo baada ya kuifunga timu ya Burundi kwa mikwaju ya penalti (6-5) kwenye uwanja wa Lugogo mjini Kampala, Uganda kufuatia timu hizo kutoka sare ya bila kufungana katika dakika zote 90 za mchezo.

Katika salamu hizo Maalim Seif alisema Zanzibar Heroes wanaendelea kudhihirisha uwezo wa Zanizbar wa kuweza kushiriki katika mashindano ya kimataifa.

 
Ameitaka timu ya Zanzibar Heroes kuongeza juhudi katika mchezo wake wa nusu fainali ili kuendeleza ushindi wake na hatimaye kuweza kutwaa Kombe hilo la Challenge katika msimu huu.

Imewekwa na MAPARA

No comments:

Post a Comment