WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, December 13, 2012

TUJIKUMBUSHE UMUHIMU WA ELIMU YA URAIA KWA TAIFA LETU


  • KWA NINI BADO TUNAHITAJI ELIMU YA URAIA KWA WATANZANIA HASA WAISHIO VIJIJINI?



Demokrasia ina gharama kubwa sana, ambayo pengine haionekani kwa haraka sana, kwa wananchi wa kawaida; mfumo huu wa maisha unawahusisha wananchi katika kutekeleza sehemu hii kubwa ya uchaguaji wa viongozi wao. Wananchi wengi hawapendi sana kujihusisha na swala hili kwa vile wanaamini kuwa sio lazima sana wao wahusike wakati kuna wengine wengi wanaweza fanya hivyo. Hivyo kila mmoja humsukumia mwenzake swala la upigaji wa kura. Kuchagua kiongozi mzuri kwao hakuna maana yeyote hii kwa kweli inatokana na dhana ya kukata tamaa, kwani katika chaguzi nyingi ambazo wamefanya, bado hawajeona faida yeyote yeyote atakayechaguliwa ni kwa ajili yao ni sio kwa ajili yetu sisi walala hoi.


Leo nitazungumzia kwa nini wananchi wengi hawajitokezi wakati wa zoezi la kupiga kura katika uchaguzi wa rais na wabunge wake: hebu tathimini tu kilichotokea katiak uchaguzi wa Raisi uliofanyika  October 2010 kumekuwa na malalamiko ya  wananchi kuto kujitokeza kwa wingi katika upigaji wa kura, swali ni kwa nini?

Mtazamo wangu unalenga zaidi katika  ukosekanaji wa elimu ya uraia;

Kwa nini tunahitaji elimu ya uraia? 

Je hatuna kabisa mashirika au idara za serikali au za watu binafsi au Mashirika yasiyo ya Kiserikali ambayo yanajishughulisha na ufundishaji wa elimu hiyo? 

Kama tunayo kwa nini hakuna mabadiliko ya msingi ya uelewa huu kwa wananchi kwa ujumla hasa wale wanaoishi vijijini? Je idara na mashirika hayo yamelenga zaidi katika ufundishaji wa elimu gani kwa ustawi wa demokrasia?

Lengo kubwa la elimu ya uraia ni kuleta na kuimarisha uelewa wa wananchi katika kuzielewa na haki zao zitokanazo na upigaji wa kura; Elimu ya uraia vile vile husaidia sana katika kuondoa fikra tofauti ambazo zinaweza kuletwa na chama au vyama katika kujinadi hasa wakati wa kampeni za uchaguzi, kama tu wananchi wameiva katika kuelewa haki zao. Wananchi hawajui hata kama wao ndio wafanyanyi wa maamuzi makubwa sana ya maendeleo yao;



Kwa nchi kama Tanzania kwa hivi sana umasikini ndio umekuwa kielelezo cha kuwachagua viongozi, ukizingatia kuwa kutokana na ugumu huo pesa utumika kununua kura, ambazo huwachagua wawakilishi wa watanzania walio wengi ambao wanakuwa hawana sauti katika kujua hatima ya maendeleo yao. Wananchi walio wengi hawana elimu kabisa ya uraia na hawajui namna gani kura zao zina thamani kwa maendeleo ya nchi. 

Kwa mfano katika wananchi takribani karibu million 19 waliojiandikisha kupiga kura ni ni pungufu ya nusu ndio waliopiga kura. Je hii inamaanisha nini?

Inaelekea kuwa elimu kama inatolewa haitolewi kwa ukamilifu hasa kwa wananchi wa vijijini, ndio maana hata leo katika nchi ya Tanzania bado kuna wananchi ambo wanafahamu fika kuwa Mwalimu J. Nyerere bado ni rais wa Tanzania; 


Je REDET wako wapi? Serikali na mashirika yake pamoja na NGOS wako wapi katika kueleimisha hili? 

Ifahamike kuwa kuto kumpa mwananchi elimu ya uraia ni kumnyanyasa kifikra na kimaendeleo. Kwa ufupi kukosekana kwa elimu ya uraia kumesababisha :

wananchi wasione umuhimu wa kwenda kupiga kura kwa kujua kuwa kupiga kwao kura ama sivyo hakuwezi kubadilisha chochote.
Wananchi hawajioni ni kama wanaweza kudai haki yao kwa njia sahihi  ya kupiga kura



Wakati umefika wa kuwauliza wote wanaohusika kwa namna moja au nyingine kwa msaada tuko kwa wafadhili au kutoka katika serikali yetu kuwawamefanikiwa kwa kiasi gani?

kwani tunafahamu kuwa kwa elimu yeyote ambayo imetolewa au itatolewa kipimo cha ufanisi au ubora wa kazi yao wanatathimini vipi?

tunaelewa kuwa kwa mwanafunzi kipimo cha elimu aliyepewa ni kuelewa alichofundishwa, kufanya tathimini  na hatimaye kuweza kufaulu mitihani yake;

Je kwa vikundi vyote vinavyojihusisha na utoaji wa elimu  hii kipimo chao ni nini kwa taifa? 

Je wanaweza kuwapimaje wale wananchi hasa wa vijijini ambao  katika marejesho yao walionyesha kuwa wamepata elimu hiyo  je ni kweli wameelewa au bado wanahitaji tena elimu zaidi  na tukizingatia kuwa wananchi wengi wa vijijini kwa bahati mbaya ya mfumo wetu ni watu wenye "pengine" wanaviwango vidogo vya elimu na pengine hata Chini ya kiwango (below Basic) na pengine hawana elimu kabisa.

wananchi wengi ambao wanaishi mijini ni wale wengi wao  wana elimu ya kutosha kuhusu mada nzima ya haki zao na nani anawafaa kuwaongoza kwa maneno mengine wamebobea katika elimu ya uraia wanaijua nini wanataka na watapata vipi na hata wanaweza kutoa ushindani kwa wanasiasa wetu.




Bado tunasafari ndefu lakini inahitaji umakini mkubwa sana; ambao unahitaji wananchi makini ambao ndio wanaweza kutuletea viongozi makini, maendeleo yetu yataletwa na sisi wenyewe na sio mtu mwingine yeyote Yule; 

Tukumbuke kuwa kama hatutachukua hatua ya haraka katika kuwaelimisha watu wetu kuhusu  elimu ya uraia tunaendelea kuwajaza wananchi wetu na ujinga hivyo na tutaendelea kuwajaza hofu katika kufanya maamuzi, hivyo hakuna namna yeyote wataweza kumchagua  mtu sahihi kwa maendeleo ya Taifa letu.

tutaishi kulalamika kuhusu vitendo vya rushwa na uchakachuaji katika chaguzi zetu; wananchi hasa wa vijijini wataendelea kuchagua Chama na wagombea ambao watakuwa na uwezo wa fedha katika dhana nzima ya ulipaji wa fadhila kwa vile ulinipa hiki name nakupa hiki. 

Lakini kama elimu ya uraia itafundishwa vyema ni rada ya kuongozea demokrasia katika nchi kwani huipeleka nchi katika njia sahihi kwa faida ya taifa na sio tija binafsi wa wanjanja wachache.

 
              Dr. Benson Bana Mwenyekiti wa REDET

Wananchi wazuri ambao wanaelewa taarifa kuhusu mwelekeo wa serikali na siasa katika nchi yao hawajezaliwa hivyo bali wamepikwa kutokana na elimu ya uraia ambayo ni kazi ya wataalamu wetu kwa kupitia misaada ya wafadhili na serikali yao kwa faida ya wananchi na sio kutumia mwanya huo kujitajirisha na kutotimiza wajibu wao wa kizalendo.

No comments:

Post a Comment