WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, December 4, 2012

UMASIKINI NI RAFIKI WA UCHAWI...!


 Picture

Na: Meshack Maganga- Iringa.

Jana usiku nilifatilia fainali za shindano la ‘Maisha Plus’ nimejifunza mengi,shindano hili limewapatia vijana uwezo wa kujiamini, nimejifunza kwamba, Kubadilika kimawazo ni  kanuni ya kuishi; mwanadamu anayeishi huku akiwa na mtazamo wa aina ile ile,  wenye matokeo yaleyale kutokana na uoga wa kutojaribu upya, kufikiri upya na kuamini upya hupoteza uthamani wake kwani hayo si maisha aliyopangiwa mwanadamu, ni maisha ya chini sana ya wanyama na viumbe vingine na si mwanadamu. 
Katika makala iliyopita nilieleza jinsi ambavyo tabia zetu na matendo yetu ndio maaduwi wetu wakubwa wa maisha yetu. Nilipata barua pepe na simu kadhaa zikishauri namna ya kuboresha makala zangu na wengine wakidai niandike kitabu.
Makala yangu ya leo ya ‘Umaskini Ni Rafiki Wa Uchawi’ nitaongelea jinsi ambavyo uchawi ni rafiki mkubwa wa umaskini na ambavyo uchawi unatesa wengi.Fuatana nami hapa.

Watu wote wanaoamini kwamba wanalogwa au wamelogwa huwa wamejifungia mahali pagumu sana kuweza kutoka. Imani kwamba, tatizo linalomkanili mtu ni matokeo ya uchawi, humganya mtu huyo kujifutia uwezo wake wa kupambana nalo au kutafuta suluhu, na kuuachia uchawi madaraka na uamuzi. Kwa kuwa uchawi hauna uwezo wowote katika kubadili chochote kwenye maisha ya mtu, matokeo ni kukwama.Kuna maeneo mengi hapa nchini ambayo watu wake hawako tayari kufanya jambo ambalo litaonyesha kwamba wamepiga hatua ya maendeleo japo kidogo ukilinganisha na wengine. Huogopa kufanya hivyo kwa kuamini kwamba watalogwa. Huogopa kusoma sana, kujenga nyumba bora na za kisasa, kubuni na kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo na shughuli zote ambazo ni za ustawi. 
 
Miongoni mwa maeneo ambayo  yamekuwa yakitajwa sana ni Tanga,Sumbawanga, wilaya za Mvomero, Newala, Tunduru na Handeni,Makete,nk. Hata hivyo, haina maana kwamba, wananchi wote wa huko huofia uchawi au hawana maendeleo, hapana. Bali ni kwamba, kuna idadi kubwa zaidi ya watu wenye kuamini hivyo kuliko maeneo mengine.
Kuwaogopa watu fulani au wa ukoo fulani kwa sababu ya imani kwamba, watu hao wanauwezo wa kuathiri vibaya maisha ya wengine, kumepelekea baadhi ya watu na jamii kubaki nyuma kimaendeleo kwa kuburuzwa na hao watu wanaowaamini kuwa wanaweza kuwaamulia kuugua au kufa na hilo likatimia.

Tunapoyaweka maisha yetu mikononi kwa uchawi na wachawi, tunakuwa tumejitoa na hivyo kuishi zaidi kama miili kuliko kuishi kama sisi. Kwa hali hiyo tunapokea kila jambo linalotutokea kama jambo tusilomudu kulifanyia chochote kwa kuwa tunaamini kwamba linahusiana na uchawi ambao tunaamini una uwezo mkubwa sana kuliko sisi.

Kuna watu leo hii ambao kabla hawajafanya jambo maishani ni Lazima wajizindike na kupata ushauri wa waganga kuhusiana na kujiweka salama kutoka kwenye kucha za wachawi. Huyu anayeulizwa au kuombwa ushauri mara nyingi  wala hata hajui kuhusu hicho anachoambiwa akizindike au akikague. Matokeo yake ni kutoa ushauri ambao hatamaye humharibia “mteja” wake kila kitu.

Maeneo ya ajira yamejaa sana visa na mikasa ya ushirikina, ambapo watu  hujikinga kwa kutumia ndumba za aina mbalimbali. Matokeo ya jambo hili ni watumishi wengi kushindwa na kuharibu au kukwama kwa njiambalimbali. Hili hutokea kwasababu, badala ya mtu kukiri udhaifu wake na kuubadili kjuwa u-bora, hutegemea ndumba kumsafishia njia. Pia hushindwa kuwa na ubunifu kwa sababu kwake,ndumba hufanya kila kitu.

Kwa ajili ya kutafuta au kulinda vyeo lakini pia hofu za kulogwa na wenzetu huweza kutufanya tukashindwa kumudu kazi zetu vizuri na badala yake kuanza kuhangaika kujihami. Vilevile hofu hizi hutujengea chuki dhidi ya hao tunaowahisi na badala ya kazi kufanyika kinachofanyika ni malumbano, visa kuharibiana sifa na hatimaye wote 
kukwama.

Kama nilivyobainisha awali, siyo watu wote ambao wanaweza kulogwa. nimetaja mifano ya wazungu, viongozi wa dini na watu wenye kujiamini katika maana yake halisi, kuwa ni miongoni mwa wale wasioweza kulogwa. Lakini ukweli mkubwa zaidi ni kwamba, kila mtu anaweza kujikinga kutoka katika kulogwa kwa kufanya mambo kadhaa. Mtaalamu maarufu wa imani za kishirikina na pepo Bruce Goldberg anajaribu  kwa njia zake  naye kushauri namna mtu anavyoweza kuepuka kulogwa.

Pamoja  na kuchanganya kwake masuala mengi kwa pamoja kiasi cha kutanza, bado anatoa ujumbe muhimu sana kuhusiana na namna mtu  anavyoweza kujikinga na uchawi au wachawi. Njia moja anayoshauri ni hii.Kukagua mazingira tunamoishi

 Bila shaka wengi wetu huwa tunaugua kutokana na sababu za kisaikolojia zitokanazo na watu wengine au mazingira tunamoishi au kufanyia kazi. Kwa mfano, mazingira ya kelele, vurugu, kukosa usalama na usiri, yanaweza kutuathiri kimwili  na kisaikolojia. Tunapoingia kwenye matatizo haya tunaweza kujikuta tukidhani tumelogwa kwa sababu maelezo ya kitabibu hospitalini yanaweza kutuambia kwamba hatuumwi.

Kwa mfano, mtu ambaye anafanyia shughuli zake kwenye eneo lenye kelele za aina mbalimbali zikiwemo za muziki, kugombana kwa watu, honi za magari, matangazo mbalimbali ya biashara na halafu kazini kwake kukawa na kufuatwafuatwa kwingi na bosi au wenzake, anaweza kupatwa na matatizo ya kimwili. Matatizo kama haya hayawezi kupatiwa tiba hospitalini kamwe.Hali hii ipo pia kwenye kukataa kwetu kukubali hali halisi, kukataa kupokea matukio ya kimaisha kama yanavyokuja baada ya juhudi zetu kukwama. Kukataa huku ni wazi kunaweza kudhuru mfumo wetu wa kufikiri na baadaye miili yetu. Tukimudu kukabaliana au kuyapokea matukio ya kimaisha ambayo kwa mazoea tunayaona ni mabaya, tunaweza kujiokoa kutoka katika kudhani matatizo yetu ni mkono wa mtu.’ 

Kwa mfano, tunapopoteza kazi, tunapofiwa, tunapoachwa na wapenzi, tunapofilisika, tuposingiziwa jambo na matukio mengine ya aina hiyo, inabidi tujue kwamba yametutokea kwa sababu ni sehemu ya maisha na siyo kwa  sababu kuna wachawi .Badala ya kuyapokea kwa uchungu, hasira na kukata tama, inabidi tuyakubali na kuanza kufikiria namna ya kukabiliana nayo kwa njia ambayo haitatugharimu zaidi. Tujue tu kwamba, maisha yasingekuwa na matukio ya aina hiyo yangekosa maana na hakuna ambaye angependa kuishi.

Kukiri kuwepo kwa nguvu siyo ya uchawi

Kwa sababu ni kweli kwamba, binadamu anazungukwa na nguvu nyingi ambazo hazijui zote, inabidi mtu akiri kwa ufahamu kuwepo kwa nguvu hizi. Kikiri kwa ufahamu ni kukubali kuwepo kwa nguvu hizo bila kuamini kwamba miongoni mwa hizo ni uchawi, kwa maana ya nguvu alizonazo binadamu mwingine kwa lengo la kumdhuru kila amtakaye.Kila nguvu inayomzunguka binadamu iko chini ya uwezo wa binadamu kama ataamua iwe hivyo, kinachotakiwa ni kujua tu namna nguvu hizi zinavyofanya kazi nay eye kuishi kwa kufuata kanuni za kimaumbile ambazo ni pamoja na kuwa na mitazamo na mawazo safi. Njia rahisi ya kuishi kwa kufuata kanuni za kimaumbile ni ile ya binadamu kuwa na mawazo na mitazamo minyoofu. Hili ni mitazamo ambayo haimuumizi, kumvunja nguvu, kumkatisha tamaa, kumtisha na kumtia wasiwasi na woga mhusika na wengine wanaomzunguka. Kwa sababu hakuna nguvu inayopotea bure, nguvu za kinyume au hasi (negative) hurudi kinyume na hivyo mtu anaweza kudhani amelogwa, kwa sababu maelezo ya kuhalalisha kupatwa  kwake na nguvu hizo hasi yanaweza kukosena. 

Kila mmoja wetu ana nguvu ndani kwake, ambazo ni kubwa sana. Nguvu hizi kwa sehemu kubwa ziko kwenye mawazo yetu. Namna tunavyojitazama, kujiamini, kutafsiri matukio, kuwatazama wengine na mazingira, hufanya  tofauti kubwa kati yetu.

Itakuwa ni kama ndoto kwetu kulogwa kama tunatumia nguvu tulizonazo vizuri. Tukijua kwamba,  tuna nguvu hizi ambazo kama tulivyosema hujpaliliwa na kukuzwa na namba tunavoweza kuishi kwa kufuata kanuni za kimaumbile, hatuwezi kudhuriwa na uchawi.

Kutoamini kabisa katika uchawi

Uchawi ni istilahi tu, haina maana yoyote yenye kushikika. Bila shaka umeshawahi kusikia watu wenye roho mbaya wakiitwa wachawi, watu wanaofanya wengine wasifanikiwe wakiitwa wachawi, watu wanaotembea na wake  au waume za watu wakiitwa wachawi na mengine ya aina hiyo.
Hii ina maana kwamba, uchawi siyo kitu Fulani maalumu, bali dhana pana, lakini yenye kulenga uharibifu. Kama tulivyojadili hapo mapema, kuna nguvu nyingi sana na za aina mbalimbali hapa  duniani, kiasi kwamba huchanganya na kukanganya. Nguvu hizi ziko chini ya mamlaka ya binadamu kwa sababu nazo zinafuata kanuni za kimaumbile. Ni pale tunapozipa nguvu hizi dhima isiyo yake, ndipo tunapoingia kwenye kuzifanya zituzidi au kutudhibiti na kututesa.
 
Moja ya njia za kuziheshimu na kuzijali nguvu hizi ni kuamini kwamba, hazipo kwa ajili ya kuleta uharibifu kwa binadamu. Tunapaswa kukumbuka kwamba, mtu kuwanga, kusafiri na ungo, kufuga fisi, kuwa na uwezo wa kutabiri ya kesho na nguvu nyingine za aina, haina maana kwamba mtu huyo anaweza kutoa uhai wetu. Tunaweza kuutoa  uhai wetu wenyewe kwa kumuogopa .
Kwa mwaka 1940, hiyo ingeweza kukubaliwa, lakini katika karne hii ya 21, haipendezi kuendelea kuamini kwamba, nguvu yoyote tusioijua ina maana ya uchawi. Hii ni kwa sababu, kwa sasa dunia imeingia mahali ambapo binadamu amekuwa akigundua haraka uwezo mkubwa alionao.


No comments:

Post a Comment