WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Sunday, December 16, 2012

Tamko La Vijana Wa CHADEMA Mkoa Wa Mwanza





KWA nafasi yangu ya Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA) Mkoa

wa Mwanza, nimelazimika kutoa ufafanuzi na kuweka kumbukumbu sawa na kutuliza

munkari ya vijana wa mkoa huu na nchi nzima kutokana na habari zilizosambazwa kwa

njia mbalimbali za upashanaji habari.

Imeripotiwa katika njia hizo za upashanaji habari kuwa BAVICHA wanataka Katibu

Mkuu wetu wa Chama, Dkt. Willibrod Slaa, aondoke madarakani na kwamba

asipoondoka, wataandaa mandamano ya kumng’oa.

Napenda kutumia nafasi hii kusema maneno machache juu ya upuuzi huo ambao kila

mtu anajua umetokana, unaratibiwa na kusimamiwa na CCM, ikiwa eti ndiyo moja ya

mikakati ya Sekretarieti ya chama hicho inayoitwa kuwa ni mpya.

Kwa nafasi yangu, mimi ndiye msemaji mkuu wa masuala yote yanayohusu BAVICHA

kwa mkoa wa Mwanza. Kwa mamlaka yangu ninaelewa fika vijana wa Mwanza

hawajawahi, wala hawana mpango wa kubeba propaganda za CCM dhidi ya

CHADEMA na viongozi wetu kuanzia ngazi ya chini hadi ya juu, akiwemo Katibu Mkuu,

Dkt. Slaa.

Natumia fursa hii kuwaondolea wasiwasi vijana wa CHADEMA mahali kokote ndani

na nje ya nchi, vijana wa Mwanza tuko imara kukilinda chama chetu na viongozi wetu

dhidi ya propaganda za CCM na serikali ambazo zina lengo ya kudhoofisha harakati za

kujenga taasisi imara inayobeba matumaini ya Watanzania kwa ajili ya ukombozi wa

awamu ya pili.

Natumia nafasi hii pia kuwataka vijana wa CHADEMA Mkoa wa Mwanza watulie,

wakisubiri BAVICHA Mkoa ifanye maamuzi kwa kuzingatia maslahi mapana ya umma

wa Watanzania na chama chetu dhidi ya hila, njama na uchu wa mtu mmoja mmoja

miongoni mwetu ambaye anaamua ‘kufika bei’ na kubeba propaganda za CCM.

Napenda kuwaambia vijana wa CHADEMA kuwa mapambano ambayo chama chetu

kinayaendesha kiasi cha kutishia CCM kuendelea kuwepo madarakani mwaka 2014 na

2015, ni mapambano ya haki dhidi ya udhalimu, ni mapambano ya matumaini dhidi ya

kukataa tama, ni mapambano ya uadilifu dhidi ya ufisadi.

Katika kusimamia masuala hayo, Katibu Mkuu CHADEMA, Dkt. Slaa akiwa mtendaji

mkuu wa chama amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha CCM inadhoofika kabisa na

CHADEMA inaendelea kuwa tumaini jipya la huru wa kweli, mabadiliko ya mfumo na

utawala, baada ya uchaguzi mkuu 2015.

Vijana wa Mwanza, kama walivyo vijana wote walio wanachama makini wa CHADEMA,

tunatambua Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992, inayosimamia shughuli zote

za vyama vya siasa nchini inasema wazi mtu aliyekuwa mwanachama wa chama X

akiamua kujiunga chama Y, ‘automatically’ anapoteza uanachama wa chama cha awali.

Lakini pia tunatambua kuwa katiba za vyama vya siasa, ikiwemo Katiba ya CCM,

zinasema wazi kuwa mwanachama wa chama hicho akijiunga na chama kingine,

anapoteza uanachama wake kwa chama hicho cha awali automatically.

Lakini pia vijana wa CHADEMA Mwanza ambao ni makini kama ilivyo kawaida ya

vijana wa CHADEMA, tunaelewa wazi na tunaweza kusimamia kauli hii, kuwa Katibu

Mkuu Dkt. Slaa tangu alipohama CCM mwaka 1995 hajawahi, kwa maana ya kila

mwaka, kwenda ofisi yoyote ya CCM kulipia kadi yake kuhuisha uanachama kwenye

chama hicho alichokiacha kinachokufa, kikisubiri kuzikwa rasmi mwaka 2014 na 2015.

Tunatambua kwamba Dr Slaa ni mwachama hai wa CHADEMA na si mwanachama wa

CCM.

Kwa namna anavyofanya kazi zake, tangu akiwa bungeni, namna alivyotaja “orodha

ya mafisadi (list of shame) iliyohusisha viongozi wa Serikali na CCM, alivyoombwa

kugombea urais na kuungwa mkono na watanzania, anavyosimamia utendaji wa

CHADEMA na kuhakikisha chama chetu kinatekeleza wajibu wake katika kila jukwaa

dhidi ya serikali ya CCM, ni kijana mpuuzi na msaliti anaweza kusimama kumnyooshea

kidole kwa kutumia propaganda za CCM na vibwagizo vya Nape Nnauye na CCM.

Natangaza rasmi kuwa BAVICHA Mwanza haijafanya maamuzi ya kuendesha harakati

zozote za kutaka Dkt. Slaa ajiuzulu, wala haitambui maandalizi ya maandamano

kwani ni batili na aliyetoa tamko la jana, Salvatory Magafu si msemaji wa vijana wa

CHADEMA Mkoa wa Mwanza, na hivyo baraza litakaa kujadili utovu huu wa nidhamu

wa kiwango na kuchukua hatua stahiki.

BAVICHA Mwanza inaheshimu taratibu za kikatiba wa viongozi kutokutuhumiana

kwenye vyombo vya habari, hivyo nimetoa kauli yangu kama Msemaji wa BAVICHA

ngazi ya Mkoa hapa Mwanza ili kuweka kumbukumbu sahihi kwa umma na maamuzi

mengine yataendelea kufanywa kwa mujibu wa katiba, kanuni, maadili na itifaki ya

chama.

Liberatus B. Mulebele.

Mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Mwanza

No comments:

Post a Comment