WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, December 4, 2012

NI STARS NA UGANDA, ZANZIBAR NA KENYA NUSU FAINALI TUSKER CHALLENGE 2012


Wachezaji wa Uganda wakimpongeza Geoffrey Kizito (anayetazama kamera amekumbatiana na Kiiza), baada ya kufunga bao kwanza dakika ya nne dhidi ya Ethiopia katika Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole mjini Kampala. Uganda ilishinda 2-0 bao lingine likifungwa na Robert Ssentongo dakika ya 60 na kwa ushindi huo, Uganda itamenyana na Tanzania Bara katika Nusu Fainali Alhamisi usiku, mchezo ambao utatanguliwa na Nusu Fainali nyingine kati ya Kenya na Zanzibar.
Abdallah Juma wa Kenya, akimdhibiti Rodrick Gonani wa Malawi katika Robo Fainali ya kwanza ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge Uwanja wa Mandela, Namboole, mjini Kampala, Uganda. Kenya ilishinda 1-0, bao pekee la Mike Barasa dakika ya 56 na sasa Harambee Stars itamenyana na Zanzibar katika Nusu Fainali keshokutwa.
Picha kwa hisani ya Bin Zubery Blog

No comments:

Post a Comment