WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Monday, December 17, 2012

MANGULA ATAKA VIJANA WASIKUBALI KUTUMIWA KUVURUGA AMANI ,ASISITIZA HATAFANYA KAZI KWA KULIPA KISASI KWA MTU


 

Magula  akiwa amebeba  zawdi alizopewa na  wazee  Njombe
 
MAKAMU mwenyekiti  wa  chama  cha mapinduzi (CCM) Tanzania bara Bw Philip Mangula  ametoa rai kwa   vyama  vya siasa nchini kuendelea  kufanya mikutano yao kwa  kunadi sera zao kwa amani na utulivu na kuacha tabia ya  kuhatarisha amani  ya Taifa kwa  kuwatumia vijana .

Mangula alitoa rai hiyo jana katika  viwanja  vya CCM wakati akiwahutubia wananchi  wa mji wa Njombe mkoani hapa mara  baada ya  kuwasili mkoani kwake kwa mara ya  kwanza  baada ya kuchaguliwa  kuwa makamu mwenyekiti  wa CCM Taifa .

Alisema kuwa amani  ambayo tunajivunia  ipo  siku  itatoweka  na iwapo  vyama  vya siasa  vitaacha kufanya kazi yake ya  kisiasa kwa kunadi  sera  za vyama  vyao na kueneza  chuki  dhidi ya  serikali kama ilivyo  hivi  sasa kwa baadhi ya  vyama kuendesha siasa  za  chuki na  kuwatumia vijana kuvuruga amani yetu.

Bila   kuvitaja  vyama  hivyo Mangula aliwataka  viongozi   wote  wa  vyama  vya  siasa  kuendelea  kuendesha  siasa  safi kama  kilivyochama cha mapinduzi na   kuwataka  vijana  wa CCM kutoiga siasa  za baadhi ya  vyama  vya upinzani siasa yenye  lengo la kuvuruga amani ya Taifa.

" Nawaombeni  sana vijana  wa CCM  kuendelea   kuonyesha mfano  kwa  vijana  wa vyama  vya upinzani na kamwe msije iga siasa vya vyama  vya upinzani siasa ya  kufanya  vurugu ..... hiyo ni siasa mbaya  sana na itakuja  kuliweka Taifa katika umwagaji damu"

Mangula alisema  kuwa  sehemu kubwa ya  viongozi  wa vyama  vya  upinzani ambao wamekuwa  wakichochoa vurugu  wana paspoti mfukoni na mara  baada ya  kuona amani  imetoweka wao hupanda  ndege  ni kukimbia mafichoni na  kuwaacha   watanzania na vijana ambao  wametumika kuvuruga amani  wakiendelea  kupoteza maisha yao.

Mbali ya  kuwataka  viongozi  wa vyama  vya siasa kutowatumia vijana hao  katika kuvuruga amani pia aliwataka vijana kutokubali siasa  chafu zenye chembe ya vurugu kwa watanzania.

Akielezea  kuhusu msimamo  wake  ndani ya  CCM alisema  kuwa mbali ya  kuwepo  nje ya ulingo kwa  kitambo kirefu ila kamwe hatafanya  kazi hiyo kwa kulipa  kisasi kwa  mtu awaye  yeyote na  kuwa atahakikisha anafanya kazi kwa  kuzingatia taratibu  zote za chama na hatakurupuka katika utendaji  wake

source: Francis Godwin blog

No comments:

Post a Comment