WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Friday, December 7, 2012

Nape achekelea ukweli wa Slaa *Ampongeza kwa kukiri kumiliki kadi ya CCM



Na Mwandishi Wetu

KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Nape Nnauye, amempongeza Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwa kukiri kumiliki kadi ya chama chao hadi sasa.


Alisema Dkt. Slaa ameanza kujifunza kusema ukweli baada ya kutambua uongo haulipi kwani kitendo cha kukiri kumiliki kadi 
ya CCM ni cha kiungwana hivyo anastahili pongezi.

Bw. Nnauye aliyasema hayo Dar es Salaam jana baada ya Dkt. Slaa kujibu tuhuma zake kuwa, wapo baadhi ya vigogo wa CHADEMA ambao wanamiliki kadi za CCM na wanazilipia hadi sasa.


“Dkt. Slaa amekiri katika vyombo vya habari kuwa anamiliki kadi ya CCM hadi sasa akidai anaitunza kama kumbukumbu muhimu hivyo ni vyema akawaeleza Watanzania kadi yake ameilipia hadi 
lini na aache kuwadanganya wenzake warudishe kadi za chama tawala wakati yeye ameendelea kuwa nayo,” alisema.

Bw. Nnauye amekiri kumheshimu sana Dkt. Slaa kama babu yake na alishtuka sana kusikia Katibu Mkuu huyo anawatuhumu baadhi ya viongozi wa CHADEMA na kudai ni mamluki wa CCM wakati yeye ni namba moja kwani anaowatuhumu hawana kadi za chama hicho.

“Nilimsikia Dkt. Slaa akiwatuhumu baadhi ya viongozi ndani ya chama chao kuwa ni mamluki wa CCM, hili linawasaidiaje Watanzania maskini.

“Kitendo hiki kimethibitisha upeo mdogo alionao katika kufikiri, huyu ni kiongozi mkubwa ambaye namuheshimu lakini anapaswa kujua yeye anaomba kuwa kiongozi hivyo lazima wananchi tumjue tabia zake,” alisema Bw. Nnauye na kuongeza;

“Viongozi wa aina yake ni janga kwa Taifa letu, usipokuwa mwaminifu kwa kidogo, huwezi kuwa mwaminifu kwa kikubwa,” alisema.

Majira

No comments:

Post a Comment