WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Monday, December 17, 2012

TUNAPOENDELEA KUMKUMBUKA DOCTOR REMMY ONGALA WASANII WANATAKIWA WAFANYE NINI?


NDIE MSANII ALIYEKUWA KIOO CHA JAMII KWA KUIMBA UKWELI HATA KAMA ULIKUWA HAUPENDEZI WENGI;

 
“Kifupi alinipa taswira ya mtu aliyeshajijenga; aliyechangia muziki wetu na kutukuza utamaduni wa Bongo ingawa hakuzaliwa hapa. Miaka yote alinisisitizia kuwa yeye ni Mwafrika na kwamba popote alipoishi au kutembea barani palikuwa nyumbani kwake. Mungu ailaze roho yake pema peponi” Fredy Macha

 

“Dk Remmy Ongala ni miongoni mwa wanamuziki wachache sana wanaoheshimika, na kuenziwa kwa uwezo wao mkubwa wa kufikiri, kubuni, kutoa burudani, nakuweka mikakati ya kuinua vipaji vyao. Licha ya uwezo mkubwa wa kutunga na kuimba nyimbo zenye kufikirisha (mantiki) Dk Remmy alikuwa muungwana na anaejua anachokifanya. Siku zote alihakikisha anatengeneza muziki bora na si bora muziki kama wafanyavyo watu wengi waliovamia tasnia ya muziki leo hii kwa lengo la kuchuma na kujipatia umaarufu. Naam, jina la Ramadhani Mtoro Ongala halitafutika kamwe katika historia ya wanamuziki nguli wa” Mwana dikala blog

 
NINI TUMEJIFUNZA TOKA KWA HAYATI REMMY ONGALA aka DOCTOR?

Ni takibrani miaka miwili tangu mwenyezi Mungu alipomwita mpendwa wetu  Doctor Remmy Ongala katika makao yake ya milele tarehe 13/12/2010.  
Swali la msingi kwa nini kifo chake kiliwagusa wengi katika masiaha yetu ya kila siku?

Majibu ya swali hili ni mengi sana kulingana na kila mtu na mtazamo wake na kwa namna ambavyo alikuwa anamfahamu na Doctor Remmy kupitia nyimbo zake na upendo wake kwa jamii iliyokuwa inamzunguka.


Kwa upande wangu nitazungumzia hasa URITHI  gani ambao Remmy ametuachia sisi kama wananchi wa Tanzania. Marehemu Remmy ametuachia jambo moja kubwa la kuwa wakweli katika kutekeleza majukumu yetu bila kumwogomba mtu yeyote Yule; ni Mwenyezi Mungu tu wa kuogopewa. Remmy alikuwa mkweli, muungwana na mwelimishaji wa aina yake. Kama Fredy Macha alivyowahi andika kuwa

“Kati ya 1988 hadi 1998 Remmy aliwaka dunia nzima. Alizunguka na Super Matimila akiimba nyimbo zilizoangalia maisha ya walala hoi, wasifu wa Mwalimu Nyerere (kwa kuondoa ukabila Tanzania) na kuchangia vita dhidi ya Ukimwi (“Mambo kwa Soksi”)”.


Aliweza kukitumia kipaji chake katika kuwatetea wanyonge kwa kupitia muziki wake, alikuwa anajitahidi sana kutoimba sana nyimbo za mapenzi na badala yake kuimba zaidi nyimbo zilizokuwa zinagusa na kueleza matatizo ya wanyonge watu wa kipato cha chini, ambao hawana sauti ambayo wakiitumia inaweza kuwasaidia kutatua mataizo yao.

Aliwahi kusema huko nyuma katika kazi zake kuwa  kuwa dunia hii ni sawa na  gereza hasa kwa wanyonge ambao hawana uwezo wa kuyafurahia maisha kwa vile hawana uwezo; hivyo wao ni wakuamuriwa tu nini wafanye ni sawa na wafungwa. Mafanikio ya wanyonge lazima yatokane na furaha ya matajiri ambao furaha yao ndio nafuu ya wanyonge na hasira yao ni kiyama kwa wanyonge.

Doctor Remmy kwa kweli Alifanikiwa sana kueleza ukweli wa maisha ya wanyonge kama umasikini, tatizo la ukimwi na namna ya kujikinga na maambukizo, ukiukwaji wa haki za msingi za binadamu, rushwa mapenzi na uvumilivu kwa kupitia muziki wake; ndio maana alikuwa na wapenzi wengi sana wa muziki wake hata ulikuwa ukitembelea kumbi za alipokuwa anatumbuiza daima zilikuwa zinawapenzi wengi wakifurahia muziki na kupata ujembe muruwa kabisa.

Nakumbuka sana ule wimbo wake wa Mambo kwa soksi ambao ulikuwa unahamasisha sana watu watumie kondom katika swala la mapenzi ili kujikinga na maambukizo ya ukimwi; wimbo huu ulionekana kupingana na maadili kwa wakati huu ya jamii ya kitanzania; lakini ukweli Doctor Remmy alikuwa miongoni mwa elimishaji wa kwanza kabisa wa ngono salama kwa jamii.


Aliitumia sanaa yake kuwa kweli ni kioo cha jamii katika kutatua tatizo. Hatukuwa tayari kuukubali ukweli huu, tukitumia kigezo ujumbe huu ulikuwa umewasilishwa kunyume na utamaduni wetu. Bila kuogopa ukweli na akijua kuwa jamii bado iko kwenye giza na serikali zetu zilikuwa bado hazifanya jazi ya kutosha katika kuwaelimisha wananchi wake madhara ya ukimwi; lakini ujumbe huu wa Remmy aliuweka bayana.

Je leo hii Jamii yetu inaelimishwa vipi matumizi ya kondumu? Sio kama alivyokuwa akielimisha mwanamuziki Remmy? Ujumbe wa picha au wa maigizo unaifikia jamii kiharaka na umakini mkubwa:

Tukubali au tukatae myonge myongee lakini haki yake mpe Remmy alikuwa ameona mbali na alikuwa anawaonyesha wanyonge haki hiyo ya gharama nafuu kwa usalama wa maisha yao;

Yako mengi ya kusema la msingi tu muziki ambao ulikuwa ukipigwa na kutungwa na Doctor Remmy ulikuwa na hisia kali za kuelimisha jamii yetu kulingana na mazingira; tutamkumbuka sana kupitia nyimbo zake: tutamkosa kwa sababu hatutapata tena mashairi na na uimbaji wa hisia kwama wake;

Mwenyezi Mungu amempa Baraka za maisha yake kwa kazi kubwa ambayo ametufanyia kwa kumuwezesha kutumia muda wake wa kutosha kabla ya kifo chake kumwimbia yeye; na kwa kulisoma neno lake kwa utulivu zaidi na kwa makini mpaka pale alipowita kwake katika mapumziko ya milele;
Kama wengi walivyosema tumempenda sana mpendwa wetu Remmy lakini Mungu alimpenda zaidi; Yeye alitoa na Yeye Ametwaa, jina lake na lihimidiwe milele. Tutaendelea kukumbuka kwa mchango wako mkubwa ambao jamii hii haitaweza kusahau.


Dr.Remmy Ongala ameandika Historia ambayo hakuna yeyote ambaye ataweza kuifuta na mchango wake utabaki palepale; ni wakati mzuri kwa wasanii wengine kufuata nmna hi nzuri ya kuelimisha jamii, na kuachana na kashfa zinazohusiha ukiukaji wa maadili na kubadilisha kabisa mwonekano wa sanaa kutoka kioo cha jamii ambaka upotoshaji wa maadili;
Sanaa inatakiwa ibaki kama kioo cha jamii.  Tutaendelea kukuenzi daima

unaweza mwangalia Dr Remmy Ongala akiwajibika


                                          Dr. Remmy akiimba kuhusu sifa za Mheshimiwa Mrema


Sehemu ya Mazishi Marehemu Dr. Remmy Ongola

 







1 comment:

  1. turuendelea kukumbuka Mkongwe wa muziki Remmy RIP kwa kuwaimbia nakuwatafutia haki wanyonge

    ReplyDelete