WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, December 6, 2012

NANI ANAFAA KUONGOZA SERIKALI ZETU MWAKA 2015?



Tukiwa tumebakisha miaka takribani mitatu, taifa letu liingie tena katika mchakato wa uchaguzi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Uchaguzi wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; nafikiri ni wakati muuafaka sasa wa kuanza kufikiri viongozi wa namna gani wanahitajika katika taifa letu hasa wakati huu ambapo nchi yetu ipo katika mawimbi ya mabadiliko ya fikra hasa kutoka mabadiliko makubwa ya Katiba katika historia ya Taifa letu.

Ni matarajio yetu kuwa uchaguzi wa mwaka 2015 pengine utakuwa na historaia ya pekee; upekee wa uchaguzi huu ni matarajio ya wananchi wengi kuwa uchaguzi huu utafanyika katika kipindi ambacho taifa litakuwa limekwisha pata Katiba yake mpya; 

swali ambalo tuanalojiuliza sasa ni je Katiba hiyo itakuwa imekizi matakwa ya Taifa ambalo linataka kusonga mbele kimaendeleo?

Kama taifa litakuwa limefanikiwa kupata Katiba bora basi hatuna budi tupate viongozi ambao kwa kweli nao watakuwa bora katika kuongoza Taifa letu kuelekea kwenye maisha bora kwa kila mtanzania. Ni ukweli ambao haupindiki kuwa Katiba bora ni msingi wa maendeleo ya nchi kwani ni msaafa wa sheria na kanuni sahihi kufuatwa na itamlazimisha kiongozi  kuongoza kwa uwajibikaji; kuonyesha uzalendo na kuwa mfano bora kwa viongozi wengine.


Pengine katika msingi huu tutahitaji kiongozi ambaye anauelewa mpana wa kuielewa Katiba ili aweze kuisimamia kwa dhati kabisa; tutahitaji viongozi wenye UWEZO wa kufikiri kwa usahihi, kuamua kwa usahihi na kutenda kwa usahihi wakitambua dhamana ya uongozi ambao taifa linawapa. Kwa hivyo tutahitaji  RAIS pamoja na mambo mengine awe na UWEZO kuongoza kwa usahihi. 

Vile vile tunahitaji viongozi wajao katika serikali zetu mbili wawe ni watu wa WATU; viongozi ambao wataweza kuona matatizo ya wananchi wao ni yao na yanawakera wanawanyima usingizi, yana wafanya waongeze nguvu ya uwajibikaji wa kusimamia rasilimali za Taifa. Nasi kama wananchi tuwe na uwezo wa kuwapima kwa watakacho kifanya wakiwa madarakani.

Pengine tutahitaji kidogo aina ya viongozi wetu wawe wakali japo sio sahihi katika nchi ya kidemokrasia kutumia msemo huu lakini wakati mwingine ile tuweze kupiga hatua ya maendeleo tutahitaji viongozi wenye mawazo ya  kidikteta ili tuweze kubadilisha kidogo maadili ya utendaji kwa  Watanzania hasa viongozi wetu katika mawizara na idara zake:Tunahitaji  Maraisi katika serikali zetu mbili ambao wanaweza  kuwawajibisha mara moja watendaji wake ambao wanashindwa kuwajibika, tuwapate viongozi ambao wanaweka pembeni huruma na urafiki ambao hauna faida kwa Taifa;

Nafikiri itakuwa ni jambo la busara kama sisi kama watanzania na wapiga kura tukiweza kuepuka tabia ya kuwachagua viongozi wetu kwa  Mazoea, Mkumbo na kwa kutumia Hisia na mapenzi binafsi juu ya wagombea. Nafikiri umefika wakati tuwachagua viongozi wetu kwa upeo wao wa kuona mambo mbalimbali nauwezo wao wa uongozi hapa nazungumzia uzoefu wa kiongozi kabla ya kuchaguliwa kuwa rais je amefanikiwa kwa kiasi gani katika idara ambayo amewahi kuongoza?

kama taifa tunafahamu kuwa taifa letu bado linaogelea sana katika tope nzito la matumizi mabaya ya rasilimali ya Taifa Rushwa na Ufisadi basi tunahitaji Rais ambaye analiona hili kuwa Lazima tukubali kuwa mabadiliko yoyote ya kisiasa, kijamii na kiuchumi yenye kulenga kuletea faida wananchi walio wengi hayawezi kufanikiwa bila ya kutokomeza rushwa na ufisadi. Kiongozi wetu aweze kuliona hili na kuwa tayari kupambana nalo akiamini kuwa Tanzania yetu tatizo la rushwa limeshaota mizizi:Watanzania wengi kwa  mamilioni wamepoteza matumaini na hali zao za maisha lakini Maraisi wetu wapya watakuwa tayari  kulitatua tatizo hili na kuwachukulia sheria wale wote ambao wamehusika katika uchafu huu,

Tunahitaji vile vile kiongozi ambaye ataweza kuyatekeleza kwa vitendo manemo haya ya Mheshimiwa Yusuph Makamba “maendeleo ya Watanzania yataletwa na wao wenyewe, kwa kufanya kazi. Watanzania wamekuwa wavivu wa kufanya kazi na kwamba kila kitu wanategemea kitafanywa na serikali … Watanzania wataendelea kulia umaskini kwa kuwa hatuna tabia ya kushirikiana na kufanya kazi,”. Kauli hii ni nzito kiongozi wetu anayetaka kuongoza taifa hili lazima awe kuwahamasisha wananchi bila kuogopa kwa kuwaeleza ukweli huu bila kuogopa kukosa kura katika kipindi kingine cha uchaguzi.


Daima tunapofikiria kuwachagua viongozi wa juu wa Taifa letu tunayakumbuka maneno ya Baba wa Taifa  Mwalimu Nyerere aliwahi sema kuwa kazi ya urais ni ngumu na inahitaji busara na kuchukua maamuzi magumu, ili kuweza kutimiza haki wananchi wanyonge “ walala hoi ”; aliendelea kushauri kuwa “Ole wale wanaokimbilia Ikulu, wanakimbilia nini, Ikulu hakuna biashara ya kufanya, Ikulu ni mahali patakatifu na kama kuna mtu anadhani kuwa kukaa Ikulu ni raha basi angeniuliza mimi katika kipindi cha miaka 21 niliyokaa Ikulu nimefanya biashara gani,Ikulu ni mzigo mzito”

Mwandishi Nyenyembe aliwahi andika kuwa “Kwa maana hiyo mtu anapoamua kuulilia urais,urais sio pambo la nchi,urais ni jalala, urais ni chumba cha kuhifadhia maiti,urais ni njaa,urais ni magonjwa,urais ni bakuli la kukingia machozi ya watu wanyonge wanaolia kila siku wakihitaji msaada na kama hawapati anayetazamwa hapo ni rais”

Je katika hawa yupi unafikira anafaa kuongoza serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  na Ile Ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanznibar ifikapo mwaka 2015: Na kwa sababu Gani?



                        Mheshimiwa DrAli Mohamed Shein


                                        Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe

                                   
                                          Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa.

                                         Dr. Wilbrod Slaa 



                                           Mheshimiwa Freeman Aikaeli  Mbowe


                                         Mheshimiwa Samuel John Sitta


Dr. Asha-Rose Mtengeti Migiro



                                          Mheshimiwa JOHN SHIBUDA MAGALE

                                         
                                        Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed


                                         Mheshimiwa Dr. Anna Kajumulo Tibaijuka


                                          mheshimiwa Dr. Mohamed Gharib Bilal


                                         Professor  Haruna Ibrahim LIPUMBA


                                         Rev. Christopher Mtikila


                                               
                             Mheshimiwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli


                                 
                                         Mheshimiwa January Makamba


                                         Mheshimiwa Bernard Kamillius Membe
                         

                                          Mheshimiwa Dr Harrison Mwakyembe,


                                     
                                        Mheshimiwa Shamsi Vuai Nahodha 


                                        Mheshimiwa Seif Sharif Hamad

                        
                         mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi

No comments:

Post a Comment