WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Monday, December 17, 2012

FILIKUNJOMBE AWACHANA VIONGOZI WAVIVU SERIKALINI NA CCM MBELE YA MANGULA



Mbunge wa  jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe (kushoto) akiwa na diwani wa Ludewa Bw Mpambalyoto wakila kiapo

 Viongozi   wa CCM mkoa  Njombe  wakishirikiana na makamu mwenyekiti wa CCM Taifa Phili Mangula ( wa pili kulia ) kuwaongoza  wanachama wapya wa CCM zaidi ya 600 waliojiunga na CCM jana wakati wa mapokezi ya makamu huyo  wa kwanza  kuli ni mbunge wa jimbo la Njombe kusini na spika  wa bunge Anne Makinda  wa tatu kutoka kulia ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga ambae ni mbunge wa jimbo la Njombe kasikazin na anayefuatia ni katibu wa CCM mkoa wa Njombe Hosea Mpangike

Makamu  mwenyekiti  wa CCM Tanzania Bara  Philip Mangula akishuka jukwaaani baada ya  kukabidhiwa dhana za kijadi na  wazee  wa mkoa wa Njombe kama nyenzo za kupambana na vitendo vya ufisadi ndani ya CCM ,Mangula alikabidhiwa dhana  hizo  katika mkutano  mapokezi yake  uliofanyika mjini Njombe (picha na Francis Godwin)
Magula  akiwa amebeba  zawdi alizopewa na  wazee  Njombe
 Mangula akikabidhiwa  vitendea kazi na mzee  wa Njombe 
 Umati  wa wananchi  waliofika  kumpokea




 Kiongozi  wa  dini  akimuombea na kumpa maneno ya  hekima
 Mangula na spika Makinda  wakiwa  wameinamisha vichwa  wakati wa maaombi maalum kutoka madhehebu yote ya dini Njombe 
 Kiapo kwa  wanachama  wapya  wa CCM 




Mapokezi ya  Mangula Njombe yatisha


Na Francis Godwin, Njombe 

MBUNGE wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Deo Filikunjombe awakuna wapiga kura wa jimbo la Njombe Kaskazini Linaloongozwa na mbunge wake Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga Kwa kuwalipua watendaji wabovu serikalini ,mbele ya makamu mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi ( CCM) Tanzania bara  Philip Mangula.

Filikunjombe ambea alipewa nafasi ya kusalimia katika mkutano huo mkubwa wa mapokezi ya Mangula mkoani Njombe alisema kuwa masikitiko ya wananchi juu ya serikali ya CCM yanatokana na baadhi ya viongozi wabovu ndani ya Chama na serikalini ambao wamekuwa wakifanya kazi chini ya kiwango na kupelekea wananchi kukichafua Chama tawala.

Hivyo alisema kuwa imani ya wana CCM kwa safu ya sasa chini ya mwenyekiti Dkt Jakaya Kikwete katibu mkuu Abdalaman Kinana na makamu mwenyekiti wa bara Mangula na makamu wake wa Zanzibar Dkt Ally Mohamed Shein na  viongozi wengine ndani ya CCM ni matumaini mapya kwa wana CCM na tishio kwa vyama vya upinzani.

" Ndugu zangu wananchi wa Makambako na mkoa wa Njombe Chama chetu CCM ni Chama kizuri sana na safu hii ya sasa chini ya Rais Kikwete ,Kinana na Mangula ni safu ya uhakika na itakiwezesha Chama  chetu kuendelea kuaminiwa zaidi na watanzania ...ila tatizo ni viongozi wachache wa serikali wasiowajibika katika nafasi zao"kauli iliyowakuna wananchi na kushindwa kujizuia kushangilia huku wakiimba wewe ni Jembe .

Hata hivyo Filikunjombe alisema kuwa ili Chama kuendelea kupendwa na akina Mangula na Kinana wanapaswa kusaidiwa na watanzania wote kwa kuombewa zaidi ili kuendelea kuifanya kazi hiyo bila woga ndani ya chama.


Kwa Upande wake  Mangula mbali ya kusifu mapokezi makubwa ya kihistoria Katika mji wa Makambako na Njombe mkoani Njombe aliweza kutoa  ya Moyoni kuhusu Kati yake na Rais Jakaya Kikwete kwa Madai kuwa yeye alikuwa hajui chochote juu ya uteuzi wake na kuwa alisitaajabu kupokea simu ya Kikwete kuhusu kusudio la uteuzi wake.

" Kweli Mimi nilikwenda Dodoma katika mkutano mkuu wa CCM Kama mualikwa ila Nikiwa Hotelini nilipokea simu ya mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Kikwete akiomba kuniteua kuwa makamu mwenyekiti na baada ya kwenda Ukumbini wajumbe wote walinipa kura zote za ndio...kweli namshukuru sana mwenyekiti wangu na wanachama wote na sasa ni kazi zaidi na sitawaangusha"


Hata hivyo aliwataka wana CCM kufanya vikao bila kuchota na kuwa wasizingizie kukosa ajenda kwani hata kukosa ajenda ndani ya CCM ni ajenda Kukosa agenda pia ni agenda ndani ya CCM pia yaweza kuwa ajenda.

Aidha amehimiza  nidhamu na taratibu ndani ya CCM kuendelea kuzingatiwa ili kukiwezesha Chama kuwa na amani na kuwa iwapo taratibu ndani ya  Chama hazitazingatiwa upo uwezekano wa Amani ndani ya nchi kutoweka.

Alisema kuwa haitapendeza kuona Tanzania inafika mahali inaendeshwa  bila Chama iwapo tutaruhusu wasiopenda Amani kuendelea kuvuruga Amani yetu iliyopo.

Mangula alisema kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa Katika katika utawala bora na kufanya mambo mengi zaidi ya kimaendeleo na iwapo wapo watu wanaosema CCM haijafanya lolote toka ilipoingia madarakani wanakionea Chama kwani maendeleo ambayo jamii inanufaika nayo sasa ni matunda ya CCM.

Awataka Vijana kupunguza jazba kwa kuwa kukubali kutumikishwa na watu wasiopenda amani ili kuvuruga amani kuwa iwapo vijana watashindwa kuepuka kutumika kwa kuvuruga amani Taifa litakwenda pabaya.

Akimkaribisha Mangula Mkoani Njombe Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga alisema kuwa CCM mkoani Njombe kimeendelea kutekeleza vema ilani ya uchaguzi pamoja na kutekeleza ahadi zake kwa wananchi.

Sang a alisema kuwa katika mji wa Makambako CCM iliahidi maji ,huduma za Afya kwa maana ya kuwa na Hospitali ya wilaya pamoja na kuwawezesha wananchi wa pembezoni kuwa na huduma ya umeme na zoezi hilo linaendelea na tayari naibu waziri wa nishati na Madini amepata kufika mjini Makambako Jana na kutembelea mradi huo.

Katibu wa CCM mkoa wa Njombe Hosea Mpangike alisema kuwa mbali ya wanachama wapya zaidi ya 1000 kujiunga na Chama hicho ila lipo kindi kubwa la wapinzani Kutoka Chadema ambao wanataka kujiunga na CCM ila wanaandaliwa mpango maalum wa kupokelewa.

No comments:

Post a Comment