WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Saturday, December 8, 2012

CUF yamtumia ujumbe maalumu Jaji Warioba



CHAMA cha Wananchi (CUF), kimetoa wito kwa Mwenyekiti wa Tume ya Kuratibu Maoni ya Wananchi juu ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba kuweka bayana muundo wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya.

Kauli hiyo ya CUF ilitolewa juzi na Katibu Mkuu wake , Maalim Seif Shariff Hamad wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Alabama Miembeni
.

Maalim Seif alisema kama Tume hiyo haikuweka bayana muundo wa mabaraza hayo na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinaweza kutumia mwanya huo kuteua wanachama wao ili wapate kulinda sera yao ya muundo wa Muungano uliopo sasa.
“Nasema hivi kwa sababu maraisi wote wawili ni wa CCM kwa hiyo wanaweza kutumia mwanya huu kuteua wafuasi wao ili wapate kutimiza idadi ya wajumbe,” alisema Katibu Mkuu huyo.

Maalim Seif ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa, alisema itakuwa jambo zuri sana kama wananchi watawekwa wazi katika kuunda mabaraza hayo.

“Naweka wazi kama kama Mabaraza haya yatakuwa na wanachama wa CCM peke yao hatuwezi kukubali abadani,” alisema Hamad.

“Lazima kuwe na uwazi na wananchi waelezwe Mabaraza hayo yataundwa na wajumbe wepi, ili kuondoa dhana mbaya inayoweza kujengwa na wananchi kuwa wajumbe hao watatoka katika chama kimoja cha siasa,” alisema Maalim Seif.Kutokana na dhana hiyo, Maalim seif aliitaka Tume ya Kukusanya maoni ya Mabadiliko ya Katiba ya Tanzania kuchukua hadhari mapema juu ya suala hilo ambalo linaweza kuharibu mchakato mzima wa maoni hayo.

Sambamba na hilo Maalim Seif alisema hata katika suala la kura ya maoni itakayokuja kufuatia huko mbele, bado kuna masuala mengine ya kujiuliza, kuhusu utaratiubu upi utatumika, wakati wa kura hiyo kwa Wazanzibari wanaoishi Tanzania Bara na watu wa Tanzania Bara wanaoishi Zanzibar.

Alieleza kuwa hofu hiyo inakuja kwa vile sheria ya mabadiliko ya katiba inasema mabadiliko hayo yatapitishwa, iwapo angalau nusu ya wananchi wa kila upande kati ya Tanzania Bara na Zanzibar wataunga mkono mabadiliko hayo, hivyo amehimiza mambo hayo lazima kwanza yawekwe wazi.
Mwananchi

No comments:

Post a Comment