WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Wednesday, December 19, 2012

JK aandaliwa M4C



Na Mwandishi wa TANZANIA DAIMA

KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), imemaliza kikao chake cha siku mbili jijini Dar es Salaam, na kuazimia kuanza Operesheni ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) kwa ajili ya kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete, atekeleze madai yao.
Katika kikao hicho, mbali na ajenda nyingine, wajumbe walipokea na kujadili taarifa ya utekelezaji kutokana na maazimio ya kikao cha dharura kilichokutana Septemba 9, mwaka huu.

Miongoni mwa maazimio hayo, ilikuwa na kupata majibu ya utekelezaji wa madai yao katika barua rasmi waliyomwandikia Rais Kikwete kupitia kwa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Baadhi ya masuala hayo ambayo yaliazimiwa ni kuwataka Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali wa Polisi Said Mwema, Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la Polisi, Kamishna Paul Chagonja, na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile wawajibike kwa kujiuzulu nafasi zao au wafukuzwe kazi.

Kwamba kwa kuzingatia kuwa, mauaji kadhaa yalitokea mikononi mwa Jeshi la Polisi, vile vile waliazimia kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda, Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Morogoro na askari waliosababisha mauaji ya raia wasio na hatia Morogoro na Iringa wafikishwe mahakamani kujibu mashtaka ya mauaji.

Chanzo chetu cha siri kutoka ndani ya kikao hicho, kilieleza kuwa wajumbe walielezwa kuwa rais amesema kuwa ataifanyia kazi barua hiyo, na hivyo CHADEMA katika kutilia mkazo, waliazimia kufanya operesheni hiyo kama shinikizo.
“Kwa hiyo kuanzia Januari mwakani, M4C itaanza rasmi ili kumshinikiza Rais Kikwete atekeleze matakwa ya barua yetu kwa kuwaondoa viongozi hao waliosababisha vifo vya raia wasio na hatia.

Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), hivi karibuni waliwaonya viongozi wa chama chake kuacha kutegemea nguvu ya Jeshi la Polisi katika kukabiliana na hoja za wapinzani.

Alisema kuwa, hoja za kisiasa zinajibiwa kisiasa, lakini akaeleza kushangazwa na hatua ya viongozi wa CCM kukimbilia kuomba nguvu ya polisi wakati wapinzani wanapoibua tuhuma dhidi ya chama hicho.
Kikao hicho cha siku mbili, mbali na kupokea taarifa hiyo kuhusu Rais Kikwete, pia kilijadili ajenda tatu ambao ni taarifa ya hali ya siasa nchini, mchakato wa mabadiliko ya katiba ya nchi na operesheni ya M4C.

Viongozi wakuu wa CHADEMA wamekuwa wakimkumbusha Rais Kikwete kujibu barua yao na kuwachukulia hatua wahusika ili kuondoa hofu ambayo imetawala kwa umma kuhusu mauaji ya raia yanayozidi kujitokeza.

Katika barua hiyo kwa Rais Kikwete, walitoa wito wakimtaka aunde tume huru ya kiuchunguzi ya kimahakama (Judiciary Commission of Inquiry) kuchunguza vifo vilivyotokea katika mazingira tata katika mikoa ya Arusha, Tabora, Singida, Morogoro na Iringa.


No comments:

Post a Comment