WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Sunday, December 16, 2012

Afrika Mlio Wa Ngoma Huwavuta Wengi!




Ndugu zangu, 


Waafrika tulio wengi tumesikia milio ya ngoma tangu tukiwa kwenye matumbo ya mama zetu. Ni pamoja na midundo ya kingoma ya akina mama wajawazito wanaotembea umbali mrefu kwa miguu.

 Hivyo, mlio wa ngoma kwa Mwafrika ni kitu cha asili yake. Mwafrika halisi anaposikia mlio wa ngoma atatafakari juu ya mlio huo. Atatatufa maana ya mdundo anaousikia; ni ngoma ya furaha au huzuni? 

Midundo mingine ya ngoma inapenyeza huzuni kwa anayeisikia, mingine inaleta furaha. Afrika kwenye ngoma unaweza kumwona anayecheza akitokwa na machozi. Kuna anayemlilia, au kuwalilia, lakini, hawako hapo ngomani. Wako mbali kabisa, yumkini wameondoka duniani miaka mingi iliyopita. 
Ni midundo tu ya ngoma ndio inayomkumbusha awapendao.

 Pichani kuna ngoma inapigwa bandani. Ni ufukwe wa Bagamoyo, jana jioni. Nilipita, nami nikasikia kwa mbali. Nikasogea karibu kusikiliza. Ilinikumbusha mbali sana. Maana, mahali hapo ilipokuwa ikipigwa ngoma ni ilipokuwa hotel maarufu ya Badeco. 

Safari yangu ya kwanza ya Bagamoyo ilikuwa mwaka 1988. Ilkuwa safari ya siku nzima ikianzia Mtaa wa Mkunguni, Kariakoo. Ni kutoka saa tatu asubuhi ya kusubiri basi. Na basi likaondoka saa tano.

 Saa kumi na mbili jioni ndipo niliingia Bagamoyo. Nilichoka sana. Kesho yake nikafika Badeco. Sikuwa hata na uwezo wa kula chakula cha Badeco. Ilikuwa hotel kubwa ya Kitalii, gharama kubwa kwenye vyumba na vyakula pia.

 Nakumbuka niliweza kunywa chai tu, lakini nilikaa muda mrefu na chai yangu,  maana nilibeba vitabu vyangu. Nilipenda sana kukaa hapo, kunywa chai na kusoma, na huku nikiiangalia Bahari ya Hindi. 

Na muda wote, kulikuwa na midundo ya ngoma ikitokea Chuo Cha Sanaa, jirani na Badeco. Na nakumbuka nimepata kukaa na kunywa chai  kwenye banda hilo inapopigwa ngoma  hivi leo.

 Tumetoka mbali. 

 Maggid, 
Bagamoyo,

No comments:

Post a Comment