WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Friday, April 19, 2013

Jeuri ya Wassira: Kibanda ni nani?

 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uratibu na Mahusiano), Stephen Wasira.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uratibu na Mahusiano), Stephen Wasira, ameitetea Idara ya Usalama wa Taifa dhidi ya tuhuma zinazowahusu baadhi ya watendaji wake kuhusika katika matukio kadhaa ya utekaji na utesaji wa raia.
Akizungumza bungeni jana jioni wakati wa kujibu hoja mbalimbali zilizotolewa na wabunge waliochangia katika hotuba ya makadirio ya bajeti ya mwaka 2013/14 ya Ofisi ya Rais, alisema haiwezekani kwa watumishi wa idara hiyo kujihusisha na matukio hayo na kueleza mafanikio mbalimbali ambayo idara hiyo imeliletea taifa.

Alihoji sababu za kulihusisha
tukio la kutekwa na kuteswa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini (TEF), Absalom Kibanda; na kuhoji 'kwani yeye ni nani?.’

Wassira alisema haiwezekani idara hiyo ikahusika kwa kuwa Kibanda hana umaarufu katika siasa za Tanzania na kusema kwamba labda wangekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, angeelewa.

Kibanda alivamiwa na watu wasiojulikana wakati akirejea nyumbani kwake, Mbezi Juu, jijini Dar es Salaam Machi 5, mwaka huu.

Katika tukio hilo, watu hao walimng’oa meno, kumkata kidole na kumharibu jicho la kushoto.

Hali hiyo ilisababisha Kibanda kulazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), baadaye katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI), jijini Dar es Salaam kabla ya kuhamishiwa hospitali ya Milpark, Johannesburg, Afrika Kusini ambako anaendelea na matibabu zaidi hadi sasa.

Kibanda alifanyiwa unyama wa kutisha unaofanana na ule aliofanyiwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Stephen Ulimboka, mwaka jana.

Hata hivyo, pamoja na kwamba Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema, ameunda timu ya makachero kuchunguza kutekwa kwa Kibanda, hadi jana siku 45 tangu kutokea kwa unyama huo, hakuna taarifa za kukamatwa kwa mtu yeyote.

Katika majumuisho ya jana, Wassira alitaja mafanikio ya Usalama wa Taifa kwamba ni pamoja na kusaidia shughuli za ukombozi Kusini mwa Afrika, kuzima njama za uhaini mapema miaka ya 80 na kutoa taarifa sahihi zilizosaidia kukamatwa kwa watu waliohusika katika shambulio la kigaidi katika ubalozi wa Marekani jijini Dar es Salaam mwaka 1998.

Pia alisema kuwa ni idara hiyo ilisaidia kufikiwa kwa kiini cha ujambazi wa kupora mabenki nchini ambao ulikuwa umepamba moto sana nchini miaka ya 2004-2006.

Wassira alisema Idara ya Usalama wa Taifa haiwezi kumfuata na kumdhuru mtu yeyote isipokuwa anayepanga njama za uhaini dhidi ya serikali.  Akizungumzia udini, alisema haujaleta athari kwa wananchi wa vijijini na mijini na kwamba bado waumini wa madhehebu yote wanashirikiana katika mambo mbalimbali.

Hata hivyo, alisema katika baadhi ya matukio yaliyotokea nchini katika miezi ya karibuni, serikali imechukua hatua kadhaa za kudhibiti matukio hayo.

Alizitaja hatua hizo kuwa ni kumkamata mtuhumiwa wa mauaji ya Padri Evaristus Mushi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Minara Miwili Zanzibar; kuwakamata na kuwafungulia mashitaka watuhumiwa wa kuchoma makanisa Mbagala mkoani Dar es Salaam pamoja na waliohusika katika vurugu za Geita na kusababisha kifo cha mchungaji.  Wassira alisema kuwa hatua nyingine ni kukamata kanda za uchochezi katika baadhi ya maeneo kama Dar es Salaam, Tanga, Simiyu na Mwanza na wahusika kukamatwa.

Alilitaka Bunge bila kujali itikadi za wabunge kukemea vitendo vya uchochezi wa dini badala ya kuchochea.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment