WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Saturday, April 20, 2013

'Bunge si patakatifu, ni pango la wanyang’anyi' -Wananchi


 
Naibu Spika John Ndugai.
Wanaharakati na wasomi wameonyesha kusikitishwa na mijadala ya matusi na lugha za kuudhi zinazotolewa na Wabunge mjini Dodoma.
Kutokana na hali hiyo, wamesema hawaoni sababu ya wabunge hao kuitwa waheshimiwa wakati hawastahili kupata nafasi hiyo kwa jamii kwani hata bungeni kwenyewe sasa si mahala patakatifu tena na badala yake ni pango la wanyang’anyi.

“Zamani kuwa mwanasiasa ni fahari, lakini sasa ni aibu na kujidhalilisha mbele ya jamii inayokuzunguka, lakini hata familia yako,” alisema mwananchi  aliyejitambulisha kwa jina la Karim Lichela.

Masikitiko hayo yalitolewa juzi usiku wakati wa mjadala uliokuwa na mada isemayo, mijadala ya wabunge iliyotawaliwa na lugha za kuudhi, kejeli, vijembe na matusi, je! Wanawakilisha  ipasavyo waliowachagua?

Mjadala huo ulioendeshwa na kituo cha televisheni cha ITV, mbali na wasomi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Ardhi, kiliwahusisha wanaharakati kutoka vituo mbalimbali likiwemo Jukwaa la Katiba na wananchi mbalimbali huku wakidai kuwa hukumu ya wabunge hao ni 2015.

Kwa ujumla wao walionyesha kusikitishwa na kauli chafu zinazotolewa bungeni huku wakikitupia lawama kiti cha Spika kuwa kimepwaya na kudai ndicho kinachoongoza  kuvunja kanuni.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba, alisema hali inayoendelea bungeni ni muendelezo wa matukio ya vikao vya bunge na kwamba halina sifa ya kuwa miongoni mwa mabunge ya Jumuiya ya Madola.

“Utakuta mbunge mmoja anazungumza, mwingine anasimama na kuomba mwongozo na hakuna utaratibu wa kupishana…” alisema na kudai kuwa wananchi waliobahatika kuzungumza nao wamediriki kusema kuwa bunge la sasa linaongozwa na mapepo.

Hata hivyo alisema inawezekana wapo wabunge wanaoendesha siasa ndani ya bunge kwa maslahi yao na viongozi kadhaa huku wakitumia muda mwingi katika kujipa umaarufu huku wakidhani wanavijenga vyama vyao.

“Wabunge wanaozuiwa ndiyo wanaowakilisha ipasavyo wananchi wao. Sasa hivi mitaani ukizungumza lugha za matusi unafananishwa na wabunge. Zinaitwa ni lugha za wabunge,” alisema na kuhoji uwezo wa kiti cha spika katika kuliendesha bunge.

Mwanaharakati mwingine, Albert Marcus, alisema Watanzania watarajie kuvuna miwa kwenye shamba la mihogo.

Alisema wabunge wamekuwa wakifanya mambo mengi ya aibu nje ya bunge na sasa wameingiza matukio hayo ndani ya bunge na kuhoji nini kazi ya kanuni zinazoliongoza bunge.
Alishauri pia ili mbunge atimize wajibu wake, hastahili kuwa kiongozi serikalini na hata mawaziri alishauri wasiwe wabunge.

Baadhi ya wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na wale wa Ardhi, walionyesha kuchefuliwa na mijadala hiyo huku wakihoji wanafunzi na watoto wadogo wanajifunza nini kutoka kwa wanasiasa hao.

Walidai kuwa jeuri wanayofanya wabunge hao inatokana na fedha za walipa kodi huku wakiwasikitikia walimu kuishi maisha magumu wakati wabunge wakichezea fedha.

Naibu Spika John Ndugai, wiki hii kwa kutumia askari wa bunge alimtoa nje ya bunge na kutohudhuria vikao vitano Mnadhimu wa Upinzani Bungeni  ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Mashariki, Tundu Lissu na wabunge wengine watano wa Chadema kwa madai ya kukiuka Kanuni za Bunge.

Wabunge wengine ni wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi,  Arusha Mjini, Godbless Lema, Iringa Mjini, Peter Msigwa,  Ilemela, Highness Kiwia na wa Nyamagana, Ezekiah Wenje.

 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment