WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, April 23, 2013

DKT. SHEIN KUTEMBELEA MIKOA YA ZANZIBAR

0 271df

Makamo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar Dkt Ali Muhammed Shein amesema kuwa ataendelea kukiimarisha na kukienzi Chama Cha Mapinduzi pamoja na kuulinda Muungano wa Serikali mbili uliopo.
Kauli hiyo ameitoa katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani wakati akizindua ziara yake ya Mikoa mitano ya Zanzibar.


Dkt Shein ambaye pia ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar amesema kuwa kuna kila sababu ya kukiimarisha chama hicho kutokana na umuhimu wake na kwamba Muungano uliopo wa Serikali mbili ndio njia bora ya kuendeleza mashirikiano ya kidugu yaliyodumu kwa muda mrefu.
Amesema kuwa lengo kuu la ziara hiyo ni kupata taarifa za matukio mbali mbali pamoja na changamoto zilizopo katika mikoa hiyo zinazohusu CCM.
Aidha amewataka viongozi wa CCM kuwa na mashirikano mazuri katika kukiimarisha Chama na kuhakikisha kwamba kinapata ushindi katika kila uchaguzi unaokuja.

Dkt. shein amesema kuwa ana imani na Chama chake kuibuka mshindi katika chaguzi kutokana Chama hicho kuchagua uongozi makini ambao utahimili vishindo vya uchaguzi ujao.
Katika hatua nyingine Dkt Shein aliwataka Wananchi kuendelea kujishughulisha na harakati zao za kujiletea maendeleo na kuepuka kuvunja sheria za nchi.

"Serikali inataka amani na utulivu kwa Wananchi wake sambamba na kuimarisha maendeleo kama Malengo ya Mapinduzi yalivyoelekeza na kwa njia hiyo hatuna budi kuyaenzi Mapinduzi" alieleza Makamo Mwenyekiti wa CCM.

Katika ziara hiyo Makamo Mwenyekiti amezindua Tawi jipya la CCM la Vikokotoni, Kikwajuni SACCOS BANK pamoja na kutoa kadi 270 kwa wanachama wapya wa Chama cha Mapinduzi.

source: Mjengwa Blog

No comments:

Post a Comment