WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, December 5, 2013

Zitto ni sikio la kufa lisilosikia dawa?
Tangu aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe na Mjumbe wa Kamati kuu, Dk Kitila Mkumbo na aliyekuwa Mwenyekiti wa mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba kuvuliwa nyadhifa zao, kumekuwa na mijadala mingi kwenye vyombo vya habari.
Ingetarajiwa kuwa Zitto na kambi yake wangetumia muda huu kutekeleza masharti waliyopewa na Kamati kuu ya chama hicho ndani ya siku 14.
Badala yake amekuwa akitumia vyombo vya habari kujitetea. Leo yupo kwenye chombo hiki kesho kile, leo gazeti hili, kesho televisheni au redio ile.
Hata kama ameonewa alitakiwa afuate taratibu ikiwa ni pamoja na kuandika barua ya kupinga uamuzi huo wa kamati kuu. Kama haridhiki zaidi, aende kwa Msajili wa Vyama vya Siasa akalalamike.
Hizo ndiyo ofisi zinazoweza kumsaidia kwa sasa, siyo kulalamika kwenye vyombo vya habari.
Ni sawa na ninaunga mkono jitihada zake ndani ya chama chao, lakini haya siyo ya kutuambia sisi. Aende kuwaambia viongozi wenzake ndani ya chama.
Huo ni udhaifu mkubwa wa Zitto kama kiongozi. Hajui wapi aseme lipi na wapi asiseme. Ni mtu anayekurupuka, hana subira wala utulivu.
Ukiangalia mifano michache tu, utaona Zitto yupo Chadema kimwili lakini kiroho yuko kwingine. Tangu mwaka 2009 alipotaka kugombea uenyekiti wa chama hicho na baadaye kushauriwa kujitoa, Zitto alianza kujitenga taratibu. Mwaka uliofuata wakati wa uchaguzi, wakati wenzake wanazindua kampeni za urais, yeye naye alikuwa akizindua kampeni za ubunge jimboni kwake tena akatangaza kuwa mwaka 2015 kuwa atagombea urais.
Kwa nini Zitto asingejumuika na wenzake kwenye uzinduzi wa kumnadi Dk Willibrod Slaa aliyekuwa akigombea urais? Au ndiyo uchu wa madaraka?
Kama hiyo haitoshi, baada ya kwenda bungeni, Zitto akataka apewe nafasi ya Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani. Kulikuwa na ulazima gani kwa Zitto kwenda kupambana na Mwenyekiti wake kwenye nafasi hiyo?
Baada ya uchaguzi mkuu, siku Rais Jakaya Kikwete alipokuja Dodoma kuzindua Bunge, wabunge wa Chadema wakiongozwa na Mbowe walisusa wakatoka nje ikiwa ni ishara kupinga matokeo ya uchaguzi.
Lakini siku hiyo Zitto hakutokea. Maswali yakazidi, je Zitto amewagomea wenzake?
Mara nyingi haonekani kwenye mikutano na operesheni za chama hicho na mawasiliano na viongozi wenzake utayakuta mitandao ya intaneti kama vile Facebook au tweeter au Jamii forum.
Kwa nini hakuwa na mawasiliano mazuri na viongozi wenzake kwenye ofisi zao, hadi ayalete kwenye mitandao ya intaneti.
Hivi leo Zitto akiwa mwenyekiti wa chama si atahamisha siri zote kwenye mitandao yote na vyombo habari? Kutakuwa na chama tena hapo?

source: mwananchi

No comments:

Post a Comment