WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Monday, December 9, 2013

WANAUME: Makali ya Kili Stars sasa yawapa presha Wakenya

wanaumeclip_87539.jpg

KENYA imeingia mchecheto na makali ya Kilimanjaro Stars na sasa imebainika kwamba Kocha Adel Amrouche ndiye aliyesisitiza mechi ikachezwe Machakos badala ya Mombasa.

Kenya itacheza na Stars kesho Jumanne kwenye mechi ya nusu fainali ya Chalenji kwenye Uwanja wa Kenyatta mjini Machakos.

Awali nusu fainali hiyo ilikuwa ichezwe hapa Mombasa, lakini kutokana na hali ya joto ambayo inaibeba Tanzania na kukaa vibaya kwa wachezaji wa Kenya wanaoishi Nairobi kwenye baridi ndio maana mechi hiyo imeahirishwa.

Baada ya mechi dhidi ya Rwanda ambapo Kenya ilishinda bao 1-0, Adel alikiri kwamba; "Hali ya hewa ya Mombasa si nzuri kwetu ni joto kiasi na wachezaji wangu hawajazoea."

Habari za ndani zinadai baada ya Uwanja wa Kisumu kushindikana kumalizika kwa wakati waandaji walipanga mechi za nusu fainali zichezwe Mombasa na fainali ikachezwe Nyayo mjini Nairobi lakini kwa hali waliyoiona katika mechi za juzi Jumamosi wenyeji wakaamua kupeleka mechi ya Stars Machakos. Mechi nyingine ya nusu fainali itachezwa mjini Mombasa.(P.T)

Habari za ndani zinadai kwamba Adel amewaambia viongozi wake kwamba endapo Kenya ikicheza na Stars mjini Mombasa itakuwa kwenye wakati mgumu kutokana na Tanzania kuzoea hali ya joto na vilevile ina sapoti kubwa Mombasa kwavile ni jirani na Tanga.
Kenya iko kwenye presha ya kufuzu fainali kwani siku ya fainali nchi hiyo itakuwa ikisherehekea Jubilee ya miaka 50 ya uhuru wake.

Wakati huohuo, Zambia iliitoa Burundi kwa penalti 4-3 katika mchezo wa robo fainali uliofanyika jana Jumapili hivyo kutinga nusu fainali.

Chanzo:http://www.mwanaspoti.co.tz

No comments:

Post a Comment