WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Monday, December 9, 2013

Hanspope:Tumemalizana na Ivo

Ivo Mapunda
Uongozi wa Klabu ya Simba umesema tayari umeshamalizana na kipa shujaa wa kupangua mikwaju ya penalti, Ivo Mapunda.
Akizungumza na NIPASHE kwa simu jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hanspope, alisema tayari wameshazungumza na nyota huyo wa Klabu ya Gor Mahia ya Kenya na atasaini mkataba nao baada ya mashindano ya Kombe la Chalenji yanayoendelea nchini Kenya.

"Baada ya kuridhishwa na kiwango chake, tulimfuata na kufanya mazungumzo naye. Tayari tumeshakubaliana naye na yuko tayari kutua Simba. Tunachokisubiri kwa sasa ni kusaini mkataba naye, atasaini baada ya michuano ya Chalenji," alisema Hanspope.

Simba imeonekana kutoridhishwa na kiwango cha kipa wake Mganda, Abel Dhaira baada ya kuamua kumsajili kwa muda wa miezi sita kipa wa zamani wa Yanga, Mghana Yaw Berko na sasa inamalizia usajili wa kipa mzawa Ivo.

Kipa huyo wa zamani wa Yanga, Ivo aliyeipa ubingwa wa Ligi Kuu ya Kenya klabu yake ya sasa ya Gor Mahia msimu uliopita, juzi alidaka penalti mbili kati ya tatu walizokosa Uganda na kuiwezesha Kilimanjaro Stars kutinga hatua ya nusu fainali ya mashindano ya Kombe la Chalenji. 

Mashindano hayo yalianza Novemba 27 na yatafikia tamati Desemba 12, mwaka huu yakishirikisha timu za taifa za nchini 11 za Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati huku mabingwa wa zamani wa Afrika, Zambia wakishiriki kama timu alikwa. 

Kanuni mpya ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) inayozitaka timu kuwa na wachezaji wa kigeni wasiozidi watatu na makipa wazawa kuanzia msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kutailazimu Simba kuachana na Dhaira na Berko na kubaki na makipa wazawa kukidhi matakwa ya Azimio la Bagamoyo.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment