WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Sunday, December 22, 2013

Profesa Ibrahim Lipumba aifunda Chadema Dar


Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetakiwa kuweka kando tofauti za kisiasa na kuunganisha nguvu zao, hasa katika kipindi hiki ambacho taifa lipo katika mchakato wa uundaji wa Katiba Mpya.
Wito huo umetolewa jana jijini Dar es Salaam  na Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba alipokuwa akifungua mkutano wa baraza kuu la chama hicho.
Alisema kuwa chama hicho chenye wabunge wengi kinapaswa kutafakari na kuweka kando itikadi za vyama na kuangalia mustakabali wa nchi katika kipindi muhimu.
“Ningependa kuwashauri Chadema kama chama chenye wawakiishi wengi bungeni kinapaswa kuweka kando tofauti za kisiasa na kuunganisha nguvu katika kwa kuangalia masilahi na mustakabali wa taifa,” alisema
“Licha ya changamoto tulizonazo hakuna sababu ya kukata tamaa mapema kiasi hiki,  tunapaswa kuondoa tofauti zetu za kisiasa a.”
Kauli hiyo ya Lipumba inakuja kutokana na vuguvugu la mgogoro ulioibuka hivi karibuni ndani ya Chadema ambao ulisababisha aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Zitto Kabwe kuvuliwa nafasi zake zote za uongozi.
source: mwananchi

No comments:

Post a Comment