WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, December 5, 2013

Samatta aivusha Bara

  Sasa kuivaa Uganda au Sudan robo fainali Chalenji

 
Mbwana Samatta wa Kilimanjaro Stars akimtoka beki wa Burundi, Ndikumana Yussuf katika mchezo wa mwisho wa Kundi C la mashindano ya Kombe la Chalenji kati timu hizo kwenye Uwanja wa Afraha mjini Nakuru, Kenya jana alasiri.
Bao pekee la dakika za mwanzo la Mbwana Samatta lilitosha kuivusha hatua ya Robo Fainali ya mashindano ya Kombe la Chalenji Timu ya Taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars), baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Timu ya Taifa ya Burundi katika mchezo wa mwisho wa Kundi B uliopigwa kwenye Uwanja wa Afraha mjini hapa jana alasiri.
Kili Stars na Zambia ndizo zilizofuzu kutoka Kundi B, baada ya Chipolopolo hao jana kushinda kwa mabao 4-0 dhidi ya Somalia katika mechi iliyopigwa jana jioni kwenye uwanja huo.

Kwa matokeo hayo Zambia sasa ndiyo inayoongoza kundi hilo baada ya timu hizo zote kuwa na pointi saba, lakini Chipolopolo wakiwazidi Kili Stars kwa wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Katika hatua ya robo fainali, sasa Kili Stars itakutana na Uganda au Sudan, lakini ratiba kamili ikitarajiwa kujulikana baada ya mechi za leo.

Akicheza kwa mara ya kwanza tangu mashindano hayo yaanze Novemba 27, mwaka huu, Samatta, mshambuliaji wa Klabu ya TP Mazembe ya DRC, alifunga bao hilo akimalizia kwa kichwa mpira wa faulo iliyochongwa na kiungo hatari wa Azam FC, Salum Abubakar 'Sure Boy' dakika ya saba ya mchezo huo uliokuwa mgumu.

Kinara huyo wa mabao katika mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika yaliyomalizika mwishoni mwa wiki huku TP Mazembe ikiambulia nafasi ya pili, pia alipiga shuti kali katika dakika ya 14 baada ya kutengewa pasi ya nje ya boksi na Himid Mao lakini kipa wa Burundi, Arakaza Arthur alipangua kishujaa kombora hilo.

Burundi, wanaojiandaa kwa mashindano ya CHAN na kuamua kuwaweka kando wachezaji wao wa kimataifa akiwamo mshambuliaji hatari wa Simba, Amisi Tambwe anayeongoza kwa mabao Ligi Kuu ya Tanzania Bara, walifanya mashambuliazi makali hasa dakika ya 23, lakini kipa Ivo Mapunda wa Kilimanjaro Stars alifanya kazi ya ziada kupangua shuti kali la Jean Nduwimana.

Kwa ushindi huo, Kilimanjaro Stars imetinga hatua ya Robo Fainali baada ya kukusanya pointi saba katika michezo mitatu ikitoka sare ya 1-1 dhidi ya mabingwa wa zamani wa Afrika, Zambia kabla ya kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya 'vibonde wa Kundi B, Timu ya Taifa ya Somalia.

Kili Stars iliwachezeha: Ivo Mapunda, Erasto Nyoni, Said Morad, Kelvin Yondani, Himd Mao, Frank Domayo, Salum Abubakar, Mbwana Samata, Mrisho Ngasa/ Ramadhani Singano (dk 81), Thomas Ulimwengu na Amri Kiemba/ Haroun Chanongo (dk 76).

Burundi: Arakaza Arthur, Hakizimana Hassan, Harerimana Rashid, Hakizimana Issa, Nsajiyumva Fredirick Duwinavyi Gael/ Moussa Mossi (dk 54), Nduwarugira Chistophe, Habonimana Celestin na Hussein Shaban/ Ndarusanze Claude (dk 58).
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment