WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, December 5, 2013

Mandela aendelea kupambana kitandani

130626094927_nelson_mandela_304x171__nocredit_689ac.jpg

Rais wa kwanza mwaafrika wa Afrika Kusini, Nelson Mandela anaendelea kupambana na ugonjwa akiwa bado kitandani, binti yake Makaziwe Mandela amesema.
Bi Makaziwe ameliambia Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini, SABC kuwa mpinzani huyo wa siasa za ubaguzi wa rangi, "bado yupo nasi, imara, na anatia moyo".
"Hata kwa kukosa neno zuri zaidi... Akiwa bado kitandani anatufundisha somo-somo la subira, upendo, uvumilivu," amesema, Makaziwe.
Bwana Mandela, mwenye umri wa miaka 95, anaendelea kupata huduma ya matibabu akiwa nyumbani kwake.
Aliruhusiwa kutoka hospitali mwezi Septemba mwaka huu baada ya kutibiwa kwa karibu miezi mitatu kufuatia maambukizi yanayojirudiarudia katika mapafu yake.
Bwana Mandela anaheshimika kwa kiasi kikubwa kutokana na namna alivyopambana dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini na baada ya kuachiliwa huru kutoka gerezani mwaka 1990 aliwasamehe wazungu wa zamani waliomkamata na kumfunga.
Alifungwa miaka 27 jela na alichaguliwa kuwa rais wa kwanza mweusi nchini Afrika Kusini mwaka 1994.
Bwana Mandela mara baada ya kumaliza kipindi kimoja cha miaka mitano ya urais, hakutaka kugombea tena nafasi hiyo.
Mwezi uliopita mke wa zamani wa Bwana Mandela Winnie Madikizela-Mandela alisema Bwana Mandela hakuweza kuzungumza kwa sababu ya mipira iliyoko kinywani ili kuvuta maji maji yaliyoko katika mapafu.
Ofisi ya rais wa Afrika Kusini mara kwa mara imekuwa ikielezea hali ya Bwana Mandela kuwa ni mahututi lakini imara
source: mjengwa blog

No comments:

Post a Comment