WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Wednesday, October 2, 2013

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI YAMUAGA BALOZI WA MAREKANI NCHINI

PIX 1  39eaa

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akimkabidhi zawadi ya ngao Balozi wa Marekani Nchini aliyemaliza muda wake, Alfonso Lenhardt (kulia) kwa ushirikiano wake aliutoa kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakati wa uongozi wake nchini. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Malimi Malemi. Waziri Nchimbi pamoja na Watendaji Wakuu wa wizara yake walimuaga balozi huyo katika Ukumbi wa Mikutano wa wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

PIX 2  37e49

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akiteta jambo na Balozi wa Marekani nchini aliyemaliza muda wake, Alfonso Lenhardt kabla ya hafla fupi ya kumuaga balozi huyo aliyemaliza muda wake wa uongozi nchini. Waziri Nchimbi pamoja na Watendaji Wakuu wa wizara yake walimuaga balozi huyo katika Ukumbi wa Mikutano wa wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.(hd)

PIX 5 e0656

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (wa pili kulia waliokaa), Balozi wa Marekani nchini aliyemaliza muda wake, Alfonso Lenhardt (wa pili kushoto waliokaa), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kulia), Naibu Balozi wa Marekani nchini, Virginia Blaser (kushoto), Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Malimi Malemi (wane kulia waliosimama) pamoja na Watendaji Wakuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya hafla fupi ya kumuaga Balozi Lenhardt. Waziri Nchimbi pamoja na Watendaji Wakuu wa wizara yake walimuaga balozi huyo katika Ukumbi wa Mikutano wa wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo. 

Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

source: mjengwa blog

No comments:

Post a Comment