WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, October 1, 2013

Ngasa aipaisha Yanga

 
Mrisho Ngassa akipenya mabeki wa timu ya Ruvu Shooting wakati timu hizo zilipomenyana jana katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana Yanga ilishinda 1-0.

Mrisho Ngasa alitoka katika kifungo cha mechi sita jana na kuichochea Yanga kupata ushindi wake wa kwanza katika mechi nne za ligi kuu ya Bara, ilipoifunga Ruvu Shooting 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa.
Kwa matokeo hayo Yanga ambayo ilikuwa imeshinda tu mechi yake ya kwanza dhidi ya Ashanti imefikisha pointi tisa kutokana na michezo sita, sawa na Ruvu ambayo imepoteza mechi ya tatu katika sita pia.
Ngasa alifungiwa na shirikisho la soka, TFF, kucheza mechi sita za kwanza za Yanga msimu huu, ukiwemo mchezo wa Ngao ya Jamii wa Agosti 17, baada ya kuonekana na hatia ya kuchukua sh. milioni 30 kwa Simba lakini akasajili Yanga.

Ilimchukua Ngasa dakika 40, hata hivyo, kuanza hatari katika lango la Ruvu alipopiga shuti kali kutoka nje ya eneo la hatari lakini likapanguliwa na mlinda mlango Abdul Seif wa timu ya wageni.
Bao la Yanga lilifungwa na Hamisi Kiiza kwa tiktaka baada ya saa moja ya mchezo, alipounganisha wavuni krosi ya Ngasa ambaye alimtoka beki wa Ruvu na mchezaji wa zamani wa Yanga Stephano Mwasika kwenye wingi ya kulia.

Kocha Ernie Brandt alisema timu yake ya Yanga ilicheza vibaya licha ya ushindi iliyopata, lakini Ngasa alicheza vizuri na kutoa mchango mkubwa katika kupata matokeo hayo.
Charles Mkwasa alisema Yanga ilitumia makosa ya timu yake ya Ruvu kupata ushindi huo.

Yanga ingeweza kwenda mapumziko ikiongoza kwa angalau goli moja kama Mganda Kiiza asingempa mpira mikononi Seif, kutokana na pasi ya akili ya Frank Domayo, katika dakika ya 39.
Tofauti na kukosa maarifa ya kufunga magoli kulikopelekea mabingwa watetezi hao kutoka sare dhidi ya Coastal Union, Mbeya City, Prisons na kufungwa na Azam kulikojitokeza katika kipindi cha kwanza, Yanga ilibadilika katika ngwe ya pili.

Kutolewa kwa Domayo anayependelea pasi fupifupi na kuingizwa kwa Athumani Iddi, kulimfanya kiungo huyo wa Taifa Stars amechezeshe zaidi Ngasa kutokana na pasi zake toka nyuma kuendeana na kasi ya winga huyo wa zamani wa Simba na Azam.

Katika mechi nyingine, Kagera Sugar iliifunga Rhino Rangers 1-0 kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Mgambo Shooting na JKT Oljoro zilitoka suluhu kwenye Uwaja wa Mkwakwani na mwanzo mzuri wa msimu wa Mbeya City uliendelea kwa sare ya 1-1 na Coastal Union kwenye Uwanja wa Sokoine.

Timu zilikuwa:

YANGA: Ally Mustafa, Mbuyu Twite, David Luhende, Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Frank Damayo (Athumani Iddi dk.50), Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Didier Kavumbagu, Hamisi Kiiza, Mrisho Ngasa.
 
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments:

Post a Comment